Picha ya mtandao
Baada ya kukamatwa na baadaye kuachiliwa, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA (Zanzibar), Salum Mwalimu, amefunguka kuwa kilichofanyika ni uonevu dhidi ya demokrasia.
Akizungumza na chombo kimocha cha habari, Mwalimu amesema kuwa kinachodaiwa na aliyetoa agizo la kukamatwa kwake kuhusiana na kutokuwa na kibali cha kufanya mkutano wa ndani hakikuwa sahihi kwa mujibu wa sheria.
Mwalimu amesema kitendo alichofanyiwa kilikuwa cha udhalilishaji na uonevu kwani, hakuwa na kosa lolote ambalo alitenda na kuongeza kuwa hata mikutano ya hadhara ya kisiasa huwa hakuna kibali bali taarifa.
Salum Mwalimu alikamatwa wakati akijiandaa kushiriki kikao cha ndani cha chama hicho, na baadaye kuachiwa bila masharti yoyote kutoka kwa Jeshi la Polisi.
No comments :
Post a Comment