Bunge la Denmark lapitisha msuada wa sheria ambao unalengo la kuwakusanya wahamiaji nchini humo na kuwaweka katika kisiwa cha Lindholm.
Msuada huo wa sheria umepitishwa Jumatano na bunge la Denmark na kutoa ruhusa kujengwa kwa kambi watakayokuwa wakizuiliwa wahamiaji katika kisiwa hicho kisichokuwa na wakazi.
Kisiwa hicho kina ukubwa wa hekari 7.
Msuada huo wa sheria umekemewa na makundi ya kutetea haki za binadamu.
Wahamiaji ambao watakuwa wamekataliwa kupewa hifadhi au wenye kukabiliwa na kesi au matendo ya uhalifu watakuwa wakipelekwa katika kisiwa hicho wakisubiri kurejeshwa kwa nguvu katika mataifa yao.
Kambi hiyo inatarajiwa kufunguliwa ifikapo mwaka 2021.
No comments :
Post a Comment