Na Thabit Madai.
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud amewataka vijana wa Mkoa huo kujiepusha na vitendo vya hanasa ikiwemo matumizi ya dawa za kulevya ili kupunguza maambukizi mapya ya ugonjwa wa ukimwi.
Mhe Ayoub ametoa wito huo wakati akifunga kongamano la siku moja la maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani kwa vijana kutoka makundi mbali mbali ya jumuiya ya umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini.
Amesema takwimu za maradhi hayo zinaonesha kuwa vijana wanatumia dawa za kulevya ndio waathirika wakubwa wa ugonjwa huo kutokana na kukosa umakini na kupelekea kupotea kwa nguvu kazi ya taifa, hivyo juhudi za pamoja zinahitajika ikiwemo utoaji wa elemu juu ya athari na kinga za maradhi hayo.Aidha Mkuu wa Mkoa amevitaka vyama vyengine vya siasa kuiga mafano wa Chama cha Mapinduzi kwa kuwapatia elimu wananchama wao hususanai vijana juu ya adhari za ugonjwa wa ukimwi ili kuendelea kuwa na vijana wenye afya bora hatimae waweze kushiriki katika shughuli za maendeleo.
Akiwasilisha maadhimio ya kongamano hilo Nd Nafdah Ali Hassan ameesema vijana wa Jumuiya za UVCCM Mkoa wa Mjini kupitia kongamano hilo waadhimia kufanyike utoaji wa elimu ngazi ya familia,familia ziwe na walezi bora kwa vijana wao, jamii iache mtazamo wa vijana kuwa ndio waathirika wakubwa,vijana wawe mabalozi kwa vijana wenzao na jamii zipunguze wingi wa mahari ili vijana weweze kuowa.
Mapema akizungumza katika kongamano hilo Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mjini Nd Kamaria Sleiman Nassor ameeleza kuwa kufanyika kwa mafunzo hayo kumeongeza uwezo na uthubutu kwa vijana na kuweza kutambua wajibu wao kwa jamii kuhusu mapambano dhidi ya maambukizi ya maradhi ya ukimwi.
Maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani hufanyika kila ifikapo tarehe 1 mwezi wa kumi na mbili ambapo kongamano hilo la vijana wa jumuiya za chama cha mapinduzi Mkoa wa Mjini lilifunguliwa naMwenyekiti wa CCM Mkoa huo Nd Talib Ali Talib.

No comments :
Post a Comment