Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, December 3, 2018

ZANZIBAR: Wanawake watumie fursa sekta ya utalii kujiendeleza kimaisha - RC Ayoub!


Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi,  Ayoub Mohammed Mahmoud amewataka wanawake nchini kuzitumia fursa mbali mbali za ajira katika sekta ya utalii ili kujiendesha kiuchumi na kuweza kupunguza utegemezi.

Ayoub ametoa wito huo wakati akifunga mafunzo maalum ya siku mbili kwa watembeza wageni wanawake yaliyoandaliwa kwa pamoja na taasisi ya ZATOGA na NVCT yaliyofanyika katika ukumbi wa Zanzibar Paradise hotel ya Aman Mjini unguja.

Amesema serikali imeendelea kupanua fursa za ajira katika sekta ya utalii,Hivyo ameeleza kuwa wanawake wana nafasi kubwa ya kuitangaza Zanzibar kiutalii endapo watahamasika kuitumia fursa ya utembezaji wa wageni kulingana na uaminifu walionao.

Aidha Mkuu wa Mkoa ameitaka kamisheni ya utalii Zanzibar kuwahamasisha wananchi hususani wanawake kuzitumia fursa za ajira katika sekta hiyo ikiwemo kutembeza wageni ili kuimarisha utalii wa kitamaduni na kuongeza kasi ya ukuwaji wa uchumi.

Hata hivyo,  Ayoub amezipongeza taasisi za NVCT na ZATOGA kwa ubunifu wao mkubwa waliouonyesha kwa kuandaa mafunzo ya utembezaji wa wageni kwa wanawake hatua ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuwasaidia kuweza kujiajiri na kupunguza changamoto zinazowakabili.

Mapema akizungumza katika ghafla hiyo,  Mkurugenzi wa Taasisi ya NVCT , Pily Khamis ameuomba uongozi wa serikali ya Mkoa wa Mjini Magharibi kwa kushirikiana na kamisheni ya utalii kuwasaidia kuwapatia usaili wa taasisi yao ili waweze kutoa huduma za mafunzo kwa makundi mbali mbali ya vijana wakiwemo wananwake kuhusu utembezaji wa wageni.

Nae mtembeza wageni wa kike, Fathiya Abdulhamid Ali amewataka wanawake wenzake kujenga utamaduni wa kujituma na kutumia fursa mbali mbali zilizopo ikiwa pamoja na kuondosha imani potofu kuwa na.Thabit Madai,Zanzibar.baadhi ya kazi haziwezi kufanywa na wanawake.

No comments :

Post a Comment