Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, January 26, 2019

DAWA YA TUNDU LISSU HII HAPA!


[4:21 PM, 1/26/2019] +1 (647) 780-9266: Anaandika kada mashuhuri wa CCM, na Mhariri wa zamani wa gazeti la SautiHuru Bollen Ngetti.
____________

DAWA YA TUNDU LISSU HII HAPA.

Na Bollen Ngetti

YULE Afisa Usalama wa TISS alimwambia Zitto, "dawa yako ni kukuua". Hii maana yake ni kwamba mbinu zote zimefeli na njia sasa inayoonekana muafaka ni kumuua Zitto. 

Inawezekana waliopanga na kuratibu mabunduki kwa Lissu nao waliona hakuna namna isipokuwa ni kumuua Lissu jaribio lililoshindwa licha kutumia risasi nyingi. Sitoshangaa kama kundi hilo la watu waovu linapanga Plan C maana kuua kulifeli, kuporwa Ubunge nao umeshindwa. Je, Tundu Lissu ameshindikana? Lakini pia tujiulize kosa hasa la Lissu ni lipi? Kukosoa Serikali? Kuna tofauti gani Kati ya Lissu na Jamal Kashoggy wa Saudia?

Nimefuatilia mahojiano ya Lissu kipindi cha "Hard Talk" cha BBC. Lissu amejitahidi sana kujibu maswali magumu ya BBC. Alichonivutia Lissu ni kwamba alikwepa kuongea uongo. Alisimamia ukweli wa alichofanyiwa na hali halisi ya siasa za Tanzania.

Dawa ya kutibu ugonjwa ws "Lissu" si kuweweseka, si kutapatapa, si kutukanana mitandaoni. Tunakosea sana wana CCM wenzangu. Lissu ajibiwe kwa hoja si vihoja. Mbona ni utamaduni wetu kujibu hoja? Wako wapi kina Nape, Mwigulu nakadhalika kumjibu Lissu? 


Lakini pia tuelewe kuwa kutokana na kunusurika kifo, imemwongezea Lissu umaarufu mkubwa wa kisiasa maana sasa anabebwa na "global sympathy" (huruma ya dunia). Hii ni hatari sana. Kama kura ingepigwa Leo ya Urais Kati ya Lissu na Magufuli kuna uwezekano Lissu angepata kura nyingi za huruma kutoka kwa kina mama ni vijana chini ya miaka 35. Kura za huruma huwa ni hatari sana maana watu hawatoangalia mema yote uliyowatendea Bali wataangalia huruma.

Uwezekano wa Lissu kugombea Urais 2020 ni mkubwa na kadri tunavyoweweseka ndivyo tunavyozidi kumpaisha. Ninachoshauri CCM tuwe makini kumpata a very strong candidate kuweza kumvaa Lissu ili tuvuke salama. Tujiulize kwa tutakayemsimamisha je, atatuvusha salama au itabidi kutumia "bao la mkono?"

Na je, "bao la mkono" litakuwa na nafasi tena katika mwanga huu ambapo dunia nzima macho yako Tanzania? Baraza la Wazee mtusaidie. Vyombo vya dola muwe "fair" kutenda haki na demokrasia. Ni vizuri JPM ashauriwe kugombea tena maana hajatangaza kufanya hivyo. Na endapo atakataa basi mgombea anayeweza kumuangusha Lissu 2020. Hiyo pekee ndio dawa ya Lissu na si kuweweseka na wito wa kumtaka arudi nyumbani. So what?

Sote tunajua mwezi wa tatu EU na USA watakata uhusiano wa kifedha na nchi yetu kwa mujibu wa taarifa zao. Sasa vijana wa Lumumba tusianze kujipanga kumhusisha Lissu na hili, hapana. Ni sisi wenyewe tumeshindwa kujenga mahusiano mazuri na mataifa haya katika kuheshimu utawala bora na haki za binadamu.

Tujiandae kisaikolojia kabla ya kufikiria "kuchapa noti hewa" kuokoa jahazi. Tujibu hoja za Lissu maana zinajibika. Msemaji wa Serikali ajitokeze kumjibu Lissu na si propaganda! Paul Makonda si size ya Lissu maana si mwanasiasa huyu. Hoja za Lissu ni za kisiasa! 

#AchaWoga2020
[4:21 PM, 1/26/2019] +1 (647) 780-9266: DUNIA INAENDELEA KUMSIKILIZA TUNDU LISSU.

Naendelea kusisitiza; Tundu Lissu hajapona ili apoe na kwenda kwao Singida au kuendelea kutulia tu kuishi na familia yake kuepuka dhahama nyingine. Damu yake haikumwagikia ardhi ya Dodoma  ili avunjike moyo na kuishi maisha ya masikitiko.

Tundu Lissu amepona kwa ajili ya mafanikio  ya Tz yenye mabadiliko, yeye akiwa kiongozi.

Watawala wapende au wasipende ndivyo ilivyo. Huko mbeleni, wakishuhudia kwa macho, watakuja kuelewa hili. Damu za wapambanaji  huwa hazimwagiki bure, wala mtu  hawezi kupata majeraha ya bure mwilini.

Lissu amevuka viwango vya mapambano.Yuko kwenye hatua ya kufanikiwa kuangamiza chama dola na mawakala wake. Ukifuatilia kwa makini Kupona kwa Tundu Lissu kumeanza kuibua kelele za watawala wanaotumia midomo ya watoto na wajukuu zao kuzungumza juu ya Lissu. Watawala wanatishwa sana na uzima wa Lissu.

Wanaijua principle ya struggle; Damu za wapambanaji huwa hazimwagiki bure.

Mpambanaji akinusurika kifo, hatima yake ni ushindi tu. WASIOJULIKANA wajue kuwa kwa ile idadi ya risasi walizotumia zilishindwa kutoa uhai wa Lissu.Hili linatudhibitishia "Mungu yuko upande wa Lissu" na hata mwacha afe bila kumaliza kazi yake ya mapambano na kuwapambania wanaoishi maisha ya kuonewa.

Hivi sasa dunia inaendelea kumsikiliza Tundu Lissu.Watu wenye akili duniani wanamsikiliza mtu aliyenusurika mauti.

 Kwanini wamsikilize Lissu ? 

 #Lissu amevuka viwango vya mapambano. Achoki Kuipigania Tanzania, sasa anatazamwa kimataifa.

Dunia itataka kujua nini jukumu  la  mtu  aliyenusurika kifo. Bila shaka Lissu atarejea Tz kupambana. Kuendelea kwake kupambana kwenye mazingira yaleyale aliyenusurika mauti, kutaishangaza dunia.

Bila kujadili kiundani alichoongea lissu kwenye kipindi cha Hardtalk kinachorushwa na BBC, yako mengi yanayoushangaza ulimwengu. Dunia inajiuliza sana maswali yafuatayo.

1.Iweje Lissu apigwe risasi nyingi kiasi hicho makao makuu ya nchi tena eneo linalotajwa kuwa na ulinzi mkali?

2.Kwanini Mpaka Leo upelelezi  haujafanyika na wahusika hawajakamatwa na kupelekwa kortini?

3.Kwanini huyu Mbunge amenyimwa haki ya kugharamiwa matibabu....?.

Ninahitimisha makala hii kwa kurejea nilichowahi andika kwenye makala nyingine juu ya Lissu; Huyu ni mtu  ambaye ameishi maisha ya kupambana Kwa ajili ya wanaonewa.

 Ameonesha uwezo na ujasiri mkubwa. Kama mtu amejitolea kutetea wanyonge wa taifa hili, hawezi kushindwa kuwaongoza akipewa dhamana 2020.

Mwanaharakati huru.

No comments :

Post a Comment