dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, January 5, 2019

MHE. BALOZI (RET. MAJOR GENERAL) ISSA SULEIMAN NASSOR AZUNGUMZA NA TANZANIAN STUDENTS" UNION IN EGYPT (TSUE)!


BALOZI (RET. MAJOR GENERAL) ISSA SULEIMAN NASSOR


TSUE HABARI:
MHE. BALOZI AHIMIZA UMOJA
Mhe. Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri, Meja Jenerali Issa Suleiman Nassor, akutana na wanafunzi wa Kitanzania wasomao katika vyuo mbalimbali jijini Cairo nchini Misri, ikiwa ni mara ya kwanza kiongozi huyo kukutana na wanafunzi hao tangu kuanza kwa mwaka mpya 2019.

Mhe. Balozi aliwaalika wanafunzi hao hapo jana, 4/1/2019, nyumbani kwake jijini Cairo ikiwa lengo ni kukutana na kuongea nao kuhusu masuala mbalimbali pamoja na kuwahimiza katika Masomo yao. Pia Mhe. Balozi Amehimiza umoja, mshikamano na kusoma kwa bidii bila kusahau kuweka malengo chanya katika maisha ya baadaye.
Mwisho alimalizia kwa kuwataka wanafunzi wote kuunga mkono na kushirikiana na uongozi katika suala zima la kuleta maendeleo katika jamii ya wanafunzi wa Kitanzania Nchini Misri.

Pia mkutano huo maalumu ulipambwa na Mhe. Balozi kwa kutoa nafasi kwa vijana wake kuuliza maswali au kutoa Maoni ambapo yaliulizwa maswali kadhaa na Mhe. Balozi kuyatolea ufafanuzi.

Pia Mhe. Balozi aliwatakia wanafunzi heri ya mwaka mpya na mafanikio katika mwaka 2019.

Idara ya Habari Na Mahusiano ya Nje ya TSUE 2018/2019 (Mhe. Khamis Mustafa Kassim)

MUNGU IBARIKI TANZANIA

No comments :

Post a Comment