dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, January 5, 2019

Mpango kazi wa vituo vya Polisi vinavyohamishika wakamilika Zanzibar!


Na Thabiti Madai, Zanzibar
Jeshi la Polisi visiwani Zanzibar, limemaliza kuratibu mpango kazi wa kuweka vituo vinavyohamishika kwa ajili ya kuimarisha usalama katika ukanda wa utalii (Mobile Police Stations).

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Yussuf Masauni, mbele ya watendaji wa wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale chini ya Waziri wao Mahmoud Thabit Kombo, ambapo ameeleza kuwa wizara yake ndio yenye dhamana ya usalama wa raia, wageni na mali zao. ,

“Nataka nikiri kwamba kuna changamoto mbalimbali katika sekta ya utalii, tuliwasilikiza wawekezaji na wadau na kukubaliana na jeshi la Polisi liandae mkakati ambao sasa uko tayari,” alieleza Masauni.

Alisema wizara yake na jeshi la Polisi kwa jumla wako tayari kushirikiana na Kamisheni ya Utalii ili kuhakikisha mpango huo unatekelezwa vizuri kwa maslahi mapana ya sekta ya utalii ambayo sasa ndio muhimili mkuu wa uchumi wa Zanzibar.

Akitoa maelezo kuhusiana na mpango kazi huo, Mkuu wa Polisi jamii na ulinzi shirikishi Zanzibar, Egyne Emmanuel, alisema kutahitajika vituo 60 ili kutoa ulinzi wa uhakika katika maeneo ya utalii Unguja na Pemba ambayo kwa jumla yana hoteli zipatazo 300.

Alisema kuwa imependekezwa utekelezaji wa mpango huo uwe kwa awamu mbili ukihusisha uanzishwaji wa vituo 30 kila awamu moja, ambapo kituo kimoja kinaweza kutoa huduma kwenye eneo lenye hoteli tano.

Alifahamisha kuwa, pamoja na mambo mengine, kila kituo kitakuwa na askari polisi mmoja na walinzi shirikishi sita watakaofanya kazi kwa shifti tatu tafauti, na pia kitakuwa na pikipiki moja kwa ajili ya doria.

No comments :

Post a Comment