Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, January 26, 2019

MSIBA WA KUSIKITISHA WATOKEA PEMBA!

Jumla ya watu sita wamefariki kutokana na chakula kinachosadikiwa kuwa na sumu katika kujiji cha Shanake kiuyu Mbuyuni wilaya ya micheweni kisiwani Pemba.

Akizungumza na wandishi wa habari, Daktari wa zamu katika hospitali hiyo, Hamad Said Hamad, alisema bado wagonjwa wengine wanne wanaendelea na matibabu.


Aliwataja wagonjwa hao kuwa ni Asma Makame Ali (12), Rashid Sadi Khatib (10), Shajiya Kombo Shoka (25) na Chumu Shiba Faki, anayekisiwa kuwa na umri wa miaka 35.

“Mmoja wa wagonjwa waliokuwa wanapatiwa matibabu alifariki jana  ambapo kwa sasa tunaendelea kuwatibu wagonjwa wanne, ambao hali zao zinaendelea vizuri, isipokuwa Asma Makame Ali, hali yake sio nzuri sana,” alisema.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na wandishi wa habari, walisema kwamba kwa kuwa waathirika hawaja tayari kutaja aina ya chakula walichokula, ni vyema serikali kuharakisha uchunguzi.

Hassan Salim Sheha (Ng’orika) mkaazi wa Tumbe, alisema kuchelewa kwa majibu ya uchunguzi kunaweza kuleta athari zaidi kwa jamii.

“Tayari watu sita tumewapoteza, hatufahamu nini kimewasibu, hivyo ni vyema uchunguzi kufanyika kwa haraka ili chanzo kifahamike na wananchi wapate matibabu sahihi,”alisisitiza.

Nae Omar Said Mohammed, alisema bado wananchi walioathirika na hali hiyo wataendelea kutokea na kusisitiza serikali kuweka kambi katika kijiji kilichoathirika ili kutoa elimu kwa wananchi.

“Nimekwambia, unaona tayari mwengine huyo anaingia bado wagonjwa wataendelea kutokea, hivyo serikali inapaswa kuweka kambi na kuwaelimisha wananchi, pengine wanaweza kusema ukweli,”alishauri.

Wengine waliofariki dunia kutoka na tukio hilo, ni Hafidh Khatib Rashid, Hifidh Khatib Rashid ambao ni watoto mapacha, Fatma Khatib Ali, Sabra Said Rashid na Hamida Bakar Rashid.

Katika maelezo yao waathirika wa tukio wametofautiana kuhusu chakula walichokula, ambapo baadhi wanadai kwamba walikula dagaa,  wengine samaki aina ya  ngogo na kasa na baadhi yao walisema walikuwa wali kwa maharage.

No comments :

Post a Comment