dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, January 5, 2019

PBZ WAZINDUA RASMI MFUMO MPYA WA KIBENKI!



Na Thabit Madai, Zanziar.

Serikali ya Zanzibar SMZ imesema kuwa kuanzishwa kwa mfumo mpya wa kibenki katika benki ya watu wa Zanzibar PBZ kutasaidia kupunguza usumbufu kwa wateja wanapotaka huduma mbali mbali.

Imesema hatua hiyo itawarahisishia wateja huduma bora kwa haraka na uhakika na kuondoa malalamiko juu ya benki hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar , Dk. Sira Ubwa Mamboya wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya wa kutolea huduma za kibenki na kuzima mfumo wa zamani, hafla ambayo iliyofanyika makao makuu ya PBZ Mperani ikiwa ni shamrashamra za miaka 55 ya mapinduzi ya 1964.

Dk, Sira mfumo wa zamani ulikuwa na changamoto kubwa ikiwemo kuzidiwa, kuwa na foleni kubwa hasa mwisho wa mwezi na kushindwa kutoa huduma nyengine za kibenki za kimataifa kama viza na master card ambapo kulikuwa kunatoa taswira mbaya kwa nchi.

Aidha aibainisha kuwa, hivi sasa benki hiyo imepata mafanikio kwa kupata faida kila mwaka kutoka mtaji usiofikia shilingi bilioni 1 kwa mwaka 2006 hadi mtaji ghafi wa shilingi 88 bilioni na mtaji wa msingi wa shilingi 70 milioni.

Hivyo, aliishauri benki hiyo kuendelea kuchukua hatua ya kujiimarisha na kuhimili zaidi ushindani wa kibiashara kwa taasisi nyengine za kifedha ambao unazidi siku hadi siku.

Akizungumzia mapinduzi, alisema yameleta manufaa na mageuzi katika mfumo wote wa kijamii na kiuchumi.

Alisema Juni 30 mwaka 1966 serikali ilianzishwa rasmi benki ya watu wa Zanzibar ambao ni uamuzi mwengine wa kimapinduzi wa kuimarisha huduma za fedha na mikopo kwa wazanzibari.

Alisema, viongozi waliopo hivi sasa wataendelea kuiendeleza na kuidumisha ili lengo la kuanzishwa liendelee kudumu.

Alitumia fursa hiyo kuwasisitiza wazanzibari kuendelea kuyalinda mapinduzi yao na kutembea kifua mbele hasa katika miaka hii ambayo inatimiza miaka 55.

Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ, Juma Ameir Hafidh, alisema kutokana na kukua kwa mfumo mpya wa teknolojia na mawasiliano, PBZ imefanya mageuzi ya kubadilisha mfumo wa zamani na kuanzisha mfumo mpya kwa lengo la kutoa huduma wakati wote.

No comments :

Post a Comment