AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, January 4, 2019

Rais Magufuli afunguka ununuzi wa korosho!

Rais wa Jahmuri ya Muungwano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema ununuzi wa korosho kwa sasa unaendelea.

Amesema hayo katika Utiaji saini mkataba wa mauziano ya mahindi kati ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na Shirika la Chakula Duniani (WFP).

'Ninafurahi hata ununuzi wa Korosho unaenda vizuri, ninajua wanao piga kelele sasa hivi ni wale wanaoitwa Makangomba kwasababu walinunua Korosho walifikiri watalipwa hela, wanapoulizwa mashamba yako wapi hawayaonyeshi," amesema Rais Magufuli.

Utakumbuka November 12, 2018  Rais Magufuli alitangaza uamuzi wa serikali wa kununua korosho zote za wakulima msimu huu kwa bei ya Tsh. 3,300 kwa kilo baada ya wanunuzi binafsi kushindwa kutimiza maaangizo ya serikali kwa kuanza kununua kwa kususua na kwa bei isiyoridhisha.

No comments :

Post a Comment