Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, January 2, 2019

RC Ayoub atoa neno Jumuiya ya wazazi CCM!


Na.Thabit Madai, Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mahamoud amewataka jumuiya ya wazazi Chama cha Mapinduzi kuwa na mchango mkubwa katika kuhakikisha wanawalea vizuri vijana na kuwa katika maadili yaliyokuwa mema.

Akifungua mkutano wa mwaka wa baraza kuu la wazazi wilaya ya dimani kichama amesema kufanya hivyo kutawezesha  vijana kuwa na heshima na taifa kuwa na nguvu kazi

Amefahamisha hatua hiyo pia itaweza kuwa na vijana wazazlendo na wenye kujitambua ili kukiwezesha chama cha mapinduzi kuwa imara  na kushinda katika chaguzi mbali mbali za chama hicho na uchaguzi mkuu ifikapo mwaka 2020.

Amesema chama cha mapinduzi ni chama chenye sera zinazokubalika, hivyo ni vyema wazazi, vijana na wananchi wote kwa ujumla kuhakikisha wanakilinda chama chao ili kuona maendeleo yanapatikana  hapa nchini.

Aidha mhe ayoub amesema serikali itaendelea kupambana na vitendo vya udhalilishaji vinavyojitokea katika maeneo mbali hatimaye vinaondoka kabisa.

Nae katibu wa jumuiya ya wazazi wilaya ya dimani kichama bw makame ameir yussuf akitoa taarifa  ya  mpango kazi ya baraza hilo amesema  jumuiya hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanapambaana na vitendo vya udhalilishaji na kuwafunza maadili mema vijana wa wilayahiyo.

Hivyo amewaomba wazazi kuwasimamia watoto wao kimalezi kwa lengo la kuwa na vijana wachapakazi na kutunza mila na silka za kizanzibar.

No comments :

Post a Comment