Ado amesema kwamba anaamini kupiti muungano wa vyama vya upinzani uliofanyika, kiongozi yoyote atakayesimamishwa kugombea urais 2020 lazima ashinde.
Akiwachambua viongozi hao wawili kwenye www.eatv.tv, Ado amesema kwamba kutokana na ukaribu wake wa kufanya kazi na Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini na hata kwenye masuala mbalimbali tofauti na kazi anamtambua ni kiongozi mwenye maono makubwa sana na Tanzania hivyo akipatiwa nafasi atafanya mambo makubwa.Akimzungumzia Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki, Ado amemuelezea kama Mwanaharakati wa siku nyingi asiyeogopeshwa lakini mwenye uwezo wa kusimama na kuikosoa Serikali ya Rais Magufuli.
"Kwa kufanya kazi nyingi na Zitto Kabwe, naweza kusema Zitto yupo tayari kubeba majukumu makubwa ya kuiongoza Tanzania. Mimi ni zao la Zitto kwenye siasa lakini pia namjua vizuri. Lakini kwa upande wa Lissu namna ninavyomtambua sina budi kusema wote wawili ni ngoma droo", ameongeza Ado.
Mbali na hayo, Ado ameshauri vyama vya upinzani kuwa havipaswi kusimamisha mgombea kila chama bali wanapaswa kuteua kiongozi mmoja atakayepewa nguvu na vyama vingine ili kuweza kuitoa serikali ya CCM madarakani.
/ EATV
No comments :
Post a Comment