Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, January 26, 2019

Viongozi wasiotimiza wajibu wao tunafyeka - RC Mwanri!


Na. Rahel Nyabali, Tabora.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri ametoa onyo kali kwa Wakurugenzi wa halmashauri za wilaya mkoani Tabora ambao wanachelewesha usajili wa wazee na kufungua madirisha ya kuwahudumia katika hospitali na zahanati kwenye maeneo wanayotokana na kusababisha adha kubwa kwa Wazee wakati wanapotafuta huduma za matibabu kwenye taasisi hizo za Serikali.

Mwanri ametoa tamko hilo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya CHF ikiwa na kaulimbiu ya Jiongeze tuwavushe salama iliyofanyika mjini Tabora kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa Wazee, Mama wajawazito na watoto.
Akizungumza katika kampeni hiyo iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali,Mkuu wa mkoa Aggrey Mwanri amewataka wananchi kuandika majina ya halimashali ambazo hazijakamilkisha usajili kwa wazee kuanzia miaka 60

“Mnakaa na watu kama hawa wa namna hiyo kwa ajili ya nini wananchi wetu wanaweza kuwa mzigo au faida, kama kunakiongizi analegalega leta jina tumfyeke iwa dakitali au nesi sema tuchukue hatua’’amesema Mwanri

Hata hivyo amesema Kuna wahudumu wana maneno machafu kwa wagojwa kwakuwambia na kuwataka wahudumu wote wa afya katika mkoa wa Tabota kuvaambulisho wawapo kazini ili kuweza kutambulika watendapo makosa

"Unakuta wazazi wanaambiwa mnazaa manazaa kama sungura mama mjamzito anaweza kumeta raisi mkuu wa mkoa anawezaje kuambiwa maneno machafu hayafai kumwambia mama mjamzito kwa sababu vifo vya wazazi vinasababishwa na uzembe’’ amesema Mwanri.

Hata hivyo amewataka wananchi mkoani humo kujiunga katika mifuko mbalimbali ya afya ili kuweza kupata huduma za afya kwa ulahisi jamba ambalo titasaidia kupunndelea guza vifo katika jamii.

No comments :

Post a Comment