dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, January 19, 2019

Wabunge wa CCM waibuka na CAG, Prof. Assad!

Wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamempongeza Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof Mussa Assad kwa kuitikia wito wa Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Mbunge wa Mbinga Mjini, Sixtus Mapunda akizungumza kwa niaba ya wabunge wa CCM amesema hatua hiyo itaendelea kuboresha ushirikiano kati ya ofisi ya CAG na Bunge.

"Tunampongeza sana CAG kwa kuitikia wito wa kamati licha ya kuwepo kwa propaganda za kwenye mitandao ya kijamii, na baadhi ya wabunge wa upinzani," amesema.

CAG, Prof Assad anatakiwa kufika mbele ya Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Januari 21, 2019 kuhojiwa kufuatia kauli aliyoitoa kwa kile alichokiita ni udhaifu wa Bunge.

Utakumbuka hivi karibuni CAG alizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa na kusema,'Kama tunatoa ripoti zinaonyesha kuna ubadhirifu halafu hatua hazichukuliwi, hupo kwangu ni udhaifu wa Bunge.

No comments :

Post a Comment