Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, January 6, 2019

Wafanyakazi elfu 3 wafutwa kazi!


Katika moja ya hatua ambazo zimechukuliwa kwenye uchumi wa Zimbabwe ni kupunguza wafanyakazi katika sekta ya umma. Vijana elfu 3 wafanyakazi wa sekta ya umma wameondolewa kazini.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya ndani nchini humo, Katibu wa baraza la huduma za jamii Jonathan Wutawunashe, amesema kwamba mishahara katika sekta ya umma imekuwa ni inachukua sehemu kubwa ya bajeti ya nchi hio, na kwa ajili hiyo basi imelazimu kuchukua hatua kwa kuchagua vipaumbele ili kupunguza gharama kwa serikali.

Katika maelezo yake Wutawunashe amesema vijana elfu 3 waliokuwa wakifanya kazi katika wizara mbalimbali nchini humo wameondolewa makazini na kwamba watu hao waliondolewa hawakufuzu vigezo vya kufanya kazi katika sekta ya umma.

Wutawunashe alisema mpango wa kupunguza wafanyakazi ni mpango wa wizara ya Uchumi na maendeleo wa mwaka 2019.Na kwamba katika kurekebisha uchumi hatua zaidi zitaendelea kuchukuliwa aliongeza.

Rais wa Zimbabwe aliyeshinda uchaguzi mwaka uliopita, tangu aingie madarakani amekuwa akipambana kuiondoa nchi hiyo katika mgogoro wa kiuchumi uliodumu kwa miaka mingi.

No comments :

Post a Comment