Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, January 2, 2019

Wananchi wapongeza hatua ya RC Ayoub kuwakamata 'madada poa'!


Na.Thabit Madai, Zanzibar
Wananchi ndani ya Mkoa wa mjini Magharib Unguja wamepongeza na kuunga mkono hatua inayochukuliwa na mkuu wa mkoa wa mjini magharib Unguja mhe, Ayoub Mohmaeed Mahomud ya kuwakamata na kuwaondoa wadada poa  wanaojihusisha na matendo ya kujiuza (ngono) katika maeneo yao.

Wanachi hao hao ni kutoka katika shehia za kikwajuni juu, kisima majongoo na mwembe shauri wameeleza hayo katika ziara maaluum iliyofanywa na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud kwenye maeneo mbali mbali ya Mkoa huo kwa lengo la kukamata watu wanaojihusisha na vitendo hivyo vya kujiuza.

Wamesema hatua hiyo ni ya kuungwa mkono kwani itasaidia kwa kiasi kikubwa kurudisha heshima na utu wa wananchi kwa kuona vitendo hivyo hauungwi mkono na kupigwa vita na kila mtu ili kuinususuru jamii hususani vijana ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakijiingiza kwa kasi katika kupatiwa huduma hiyo ambayo haiendani na mila,silka na utamaduni wa nchi.

Akizungumza mara baada ya ziara hiyo Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud amesema zoezi hilo la kuondosha machangudoa pia litahusisha kuwakamata wamiliki na wapangaji wa nyumba ambazo zimebainika kuhusika kwa biashara hiyo na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Amesema jumla ya wapangaji ishirini akiwemo mmiliki mmoja wa nyumba zinazojihusisha na masuala hayo ya ukahaba wamekamatwa na kufikishwa katika kituo cha polisi Madema usiku wa kuamkia leo huku taratibu za kisheria zikiendelea kuchukuliwa dhidi yao na zoezi hilo litaendelea nyumba hadi nyumba ili kumaliza tatizo hilo.

Mhe Ayoub amesema mmiliki wa nyumba namba125 horofa ya tano iliyopo michenzani block namba moja  Khamis Haji Mussa maarufu mista X,amesema nyumba yake imekuwa ikitumika na uwekaji wa watu wanajihusisha na vitendo vya ukahaba na ombaomba kwa kipindi kirefu kinyume na utaratibu jambo ambalo Serikali ya Mkoa imekuwa ikilikataza kwa kipindi kirefu.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Thobias Sedayoka amesema jeshi la polisi katika Mkoa huo litaendelea kusimamia zoezi hilo kikamilifu ili kuona vitendo hivyo vinavyoharibu sifa na utu wa wananchi wa Mkoa huo vinaondoka kabisa,Hivyo ametoa wito kwa baadhi ya wananchi wanaojihusisha na biashara hiyo kuacha mara moja huku akiitaka jamii kuendelea kushirikiana na jeshi hilo kudhibiti vitendo hivyo.

Jumla ya 7 na watu ishirini wa Shehia ya kisima majongoo,Kikwajuni juu na Muembeshauri na wameshikiliwa na jeshi la polisi kufuatia operasheni hiyo ya kuondoa watu wanaojihusisha na vitendo vya mmong'onyoko wa maadili katika Mkoa wa Mjini Magharibi.

No comments :

Post a Comment