Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, February 6, 2019

Jeshi la Polisi lavamia na kuwapiga maafisa wa ZAECA!

Na.Thabit Madai Zanzibar.
Jeshi la Polisi Zanzibar limedaiwa kuvamia Ofisi za Mamlaka ya kuzuia Rushwa na Kuhujumu uchumi Zanzibar (ZAECA) Zilizopo Vuga na kuwapiga maafisa wa mamlaka hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizofika kwa waandishi wa habari zinaeleza kuwa Jeshi la Polisi juzi lilivamia Ofisi za Mamlaka  hiyo na kuwapiga na kuwachukua baadhi ya maofisa wa ZAECA kwa kuwafunga pingu na kuwapeleka kituo cha polisi kilichopo Madema Mjini Unguja.

Akikiri kutokea kwa tukio hilo Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar  Mohamed Hassan haji Alisema kwamba tukio hilo limetokea juzi na kwasasa lipo kwenye meza kwa lengo la kusuluhishwa  kwa njia ya mazungumzo kati ya maafisa wa jeshi la polisi na maafisa wa ZAECA.
“Ni kweli hili suala lilitokea na sasa hivi tunalisuluhisha kwa njia ya mazungumzo kati yetu na wenzetu wa ZAECA kwa sababu hizi taasisi zipo kwa mujibu wa sheria na hakuna haja ya kuvutana kwa hivyo tunalizungumza na tutapata suluhisho” alisema Kamishna huyo.

Awali Maafisa wa Mamlaka ya kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi wanadaiwa walimuwekea mtego mmoja wa Askari wa Jeshi la Polisi na kumshika na Rushwa jambo ambalo limechochea hasira kwa jeshi hilo kutokana na mwenzao huyo kukamatwa na mtego na kwenda kutoa kichapo kwa maafisa wa ZAECA kwa madai kwamba wamedhalilishwa kukamatwa mwenzao.

“Kwa ufupi wamekuja gari mbili za Defenders hapa na kwa kishindo wakiwa na yale mavazi yao na silaha wakaingia ndani na kuwakamata maafisa wa ZAECA lakini kishindo kilikuwa kikubwa watu wengine wakataharuki na wengine wakakimbia nje wengine ndio wakaingia Ikulu na katika maeneo ya  Ikulu watu waliokuwa nje na walinzi walishituka sana” alisema mmoja wa mashuhuda.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya kupambana na Rushwa na uhujumu uchumi Zanzibar ZAECA Mussa Haji Ali hakuwa tayari kulizungumza suala hilo licha ya kwamba limempa mshituko na hofu.

No comments :

Post a Comment