Hotuba ya Rais
wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Bibi Fatma
Amani Karume – Dar es Salaam Tarehe 06 Februari
2019.
Mheshimiwa
Dr.John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa
Prof. Ibrahim Juma, Jaji Mkuu, Mheshimiwa Spika
wa Bunge la Tanzania, Waheshimiwa Majaji wa
Mahakama ya Rufani,
Waheshimiwa
Majaji wa Mahakama Kuu, Waheshimiwa
Wasajili wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu,
Waheshimiwa
Mahakimu,
Mheshimiwa Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, Ndugu Wanasheria wasomi wenzangu,
Mabibi na
Mabwana.
Tangu
utotoni nimefundishwa kwamba vilivyokuwemo kwenye
mkoba wa mwanamke ni siri yake. Bibi,
Mama au Shangazi akikutuma kumletea mkoba
wake, kwetu ilikua marufuku kuchungulia ndani.
Leo, nitaivunja
miiko kwa kuwaeleza vichache ninavyobeba kwenye
mkoba wangu: miwani, maana sioni vizuri,
rangi ya mdomo hii ni muhimu,
kipepeo, Dar kuna joto kali, na wanaonijua
vizuri wanafahamu ukikuta pesa kwenye Mkoba
wangu ni bahati.
Lakini
sitoki bila ya kubeba Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sitaweza
kugawa kila kilichopo ndani ya mkoba
isipokua matamshi ya Katiba. Na ningependa
kuanza hotuba yangu kwa kuwakumbusha Utangulizi
na Misingi ya Katiba yetu. Katiba inaanza na
utangulizi ufuatao:
“Kwa kuwa
sisi wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati
kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi
ya UHURU, HAKI, UDUGU na AMANI: Na kwa
kuwa misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa
katika jamii yenye demokrasia ambayo serikali
yake husimamiwa na Bunge lenye wajumbe
waliochaguliwa na linalowawakilisha wananchi, na
pia yenye Mahakama huru zinazotekeleza
wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo
wowote, na hivyo kuhakikisha kwamba haki
zote za binadamu zinadumishwa na kulindwa,
na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu.
Kwa hiyo
basi, Katiba hii imetungwa na Bunge
Maalum la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
kwa niaba ya Wananchi, kwa madhumuni ya
kujenga jamii kama hiyo, na pia kwa
ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa
na Serikali yenye kufuata misingi ya Demokrasia
na Ujamaa. “Misingi ya Katiba yetu
ni UHURU, HAKI, UDUGU, AMANI, DEMOKRASIA NA
UJAMAA.
Ni muhimu
pia kutambua kuwa neno Demokrasia limetajwa
mara mbili katika utangulizi huu. Na
waliotunga Katiba walielewa kwamba Mahakama
huru inayotoa haki bila woga wala upendeleo
wowote ina hakikisha haki zote za binadamu
zinadumishwa na kulindwa na ina umuhimu
wa pekee kwenye kulinda misingi ya katiba.
Nimeelezwa
kwamba uongozi wa Mahakama umeamua kauli
mbiu ya mwaka huu kuwa ni : “Utoaji
wa Haki kwa Wakati: Wajibu wa Mahakama na
Wadau”, na nimeambiwa nijikite kwenye mada hiyo. Nitaanza na
Wajibu wa Mahakama na nitamalizia na
wajibu wa wadau.
Wajibu wa
Mahakama.
Wajibu wa
Mahakama umewekwa wazi kwenye Katiba yetu. Ibara
107A (1) inasema, “Mamlaka yenye kauli ya
mwisho ya utowaji haki katika Jamhuri ya
Muungano itakuwa ni Mahakama”.
Ibara ya 107A(2)(b) ya
Katiba inaeleza “Katika kutoa uamuzi
wa mashauri ya madai na jinai kwa
kuzingatia sheria, Mahakama zitafuata kanuni zifuatazo,
yaani- a) Kutenda haki kwa wote bila
ya kujali Hali ya mtu, kijamii au kiuchumi;
b) kutochelewesha haki bila sababu ya
kimsingi; c) kutoa fidia ipasavyo kwa watu
wanaoathirika kutokana na makosa ya watu
wengine, na kwa mujib wa sheria mahususi
ilioyotungwa na Bunge; d) kukuza na
kuendeleza usuluhishi baina ya wanaohusika katika
migogoro. e) kutenda haki bila ya
kufungwa kupita kiasi na masharti ya
kiufundi yanayoweza kukwamisha haki kutendeka.”
Ibara 107B
“Katika kutekeleza mamlaka ya utoaji haki,
mahakama zote zitakuwa huru na zitalazimika
kuzingatia tu masharti ya Katiba na yale
ya sheria za nchi.” Kwa hiyo wajibu wa Mahakama ni
kutoa HAKI.
Hadithi
hadithi……….. Hapo zamani za kale, kulikua
na familia ina baba, mama na watoto
watatu, wawili wakiume na mmoja wa
kike. Watoto wakiume wakaoa wakapata
watoto. Mtoto wa kike naye akaolewa
lakini hakupata bahati ya kuzaa. Kwa furaha
kubwa Baba na mama wakawa Babu na
Bibi, na mtoto wa kike akawa
Shangazi. Muda ukapita, Babu na Bibi
wakafariki na wakaacha mali kama mashamba
na nyumba. Familia ikakaa kikao na
wakaamua msimamizi wa mirathi awe Shangazi.
Mirathi
ikafunguliwa, na Shangazi akawa msimamizi kwa
hiyo mashamba na nyumba yakaingizwa kwenye
jina lake kama msimamizi wa mirathi, lakini
kaka zake wawili wakachukua na kuendeleza
mashamba ya vijijini naye akawa anaishi
kwenye nyumba ya Babu mjini.
Maisha
yakaendelea kama kawaida bila ya ugomvi
wowote maana familia hii ilikua ina upendo
sana. Kila wakivuna shambani kaka zake wakawa
wanamtumia mazao Shangazi mjini naye Shangazi
akawa anawasimamia kazi zao za kisheria huko mjini.
Muda ukapita, wale kaka wawili nao
wakafariki, mume wa Shangazi naye akatangulia
mbele ya haki na Shangazi akabaki
peke yake kwenye nyumba ya Babu mjini.
Siku moja
Shangazi akatuma ujumbe kijijini kwa watoto
wa kaka zake waje haraka kumuona.
Walivyosikia wito wa Shangazi, wale watoto
wakaenda mjini kumtembelea. Kufika wakamkuta
Shangazi anababaika kwa huzuni. Akawaeleza
kwamba katapeliwa. Wakamuuliza “Umetapeliwa
vipi?” Akasema “Tangu alivyofariki mume wangu
nimejisikia mpweke sana. Sasa kuna dada,
aitwaye Mtu Mwema akawa ananitembelea mara
kwa mara. Siku moja nilipokua ninaumwa akanipa
karatasi ili niweke sahihi alinilaghai kuwa
ninaweka sahihi kwenye makaratasi ili kumuwezesha
yeye anisimamie kupata matibabu. Mimi nikatia
sahihi.
Juzi
nilikua natafuta hati ya hii nyumba
na sijaiona. Naogopa Mtu Mwema
kanitapeli”. Akaanza kulia. Watoto
wakatafuta mwanasheria naye alipofanya utafiti Wizara
ya Ardhi, huyo mwanasheria akakuta nyumba
ya babu iko kwenye jina la Mtu Mwema
kwa madai kapewa na Shangazi out of
love and affection “kwa UPENDO”. Mwanasheria
msomi akatoa vitabu vyake, akatoa sheria
zake akasoma. Alivyomaliza akawaambia
watoto “Hii kesi ni rahisi sana maana
kwenye sheria yetu, kifungu cha 25(1)(a)
cha Sheria ya Mikataba huwezi kumpa mtu
nyumba aliyekuwa sio ndugu yako wa damu
au ndugu wa kupitia ndoa yako kwa
UPENDO eti bila ya kulipwa senti moja.
Mkataba
huo unakua haramu na hautokubaliwa na
Mahakama”. Akawaeleza watoto kwamba hiyo sheria
iko ili kuwalinda watu wasitapeliwe.
Watoto wakamwambia Shangazi asijali maana sheria
iko upande wake na kuna Mahakama itakayotii
na kutoa haki. Kesi ikafunguliwa ikaenda miaka
3, jaji akahamishwa. Kesi ikasimama miaka 2
maana Mahakama ikawa haina majaji wakutosha.
Miaka 5 baada ya kesi kufunguliwa ikapata
jaji mpya. Kesi ikaendelea. Baada ya miezi
michache, mara Shangazi akafariki.
Kesi
ikasitishwa tena maana sasa haiwezi kuendelea
mpaka watoto wafungue mirathi ili baada
ya kuteuliwa na mahakama msimamizi wa
mirathi ya Shangazi aendelee na kesi.
Watoto wakafungua mirathi, Mtu Mwema
akapinga mirathi akataka yeye awe msimamizi
wa mirathi. Kesi ya mirathi ikaenda miaka
5. Jaji wa kwanza kwenye kesi ya
mirathi akahamishwa akaingia jaji mwengine.
Alivyoingia
jaji huyu Mtu Mwema akatoa pingamiza yake
ya mirathi ya Shangazi, na Mahakama
ikaamua mtoto wa kiume asimamie mirathi ya
Shangazi, huku ikamlaani sana Mtu Mwema kwa
kuchelewesha mirathi ya Shangazi pasipo sababu.
Huyu mtoto akachukua hati yake ya usimamizi
wa mirathi ya Shangazi akaenda mahakamani
ili kuendelea na kesi ya awali ya
Shangazi dhidi ya Mtu Mwema.
Kufika
Mahakamani Mtu Mwema akaweka pingamiza kusema
kama Kesi ya Shangazi itupwe kwa
sababu imechelewa sana kuendelea. Pingamizi
lake likakubaliwa na kesi ikatupiliwa mbali
baada ya miaka 17. Mtoto akaamua
kukata rufaa. Alipopewa makabrasha kutoka
Mahakamani akakuta kuna nakala za Ushahidi
hajapewa.
Alipouliza akaambiwa
na Msajili makabrasha ya Ushahidi yamepotea.
Miaka 15 ikapita bado kesi haijakamilika,
makabrasha ya Ushahidi yamepotea mahakamani,
mtoto nae kazeeka na kapata mshtuko wa moyo.
Sasa tujiulize kesi kama hii inaweza
kutokea kwenye nchi yenye Mahakama huru
zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila
woga wala upendeleo na kutochelewesha haki bila ya
sababu za msingi?
Kwa maoni
yangu, na naamini mtakubaliana na mimi
kuwa kesi kama hii haiwezi kutokea kwenye
Mahakama inayotekeleza majukumu yaliyoko kwenye ibara
ya 107(A) ya Katiba yetu. Kwanza kwa sababu (1)
Mahakama yetu inatakiwa kutoa HAKI; (2)
kutochelewesha utoaji wa Haki bila ya
sababu ya kimsingi na (3) pia kutenda haki
bila kufungwa kupita kiasi na masharti
ya kiufundi yanayoweza kukwamisha haki kutendeka.
Majukumu ya Mahakama yetu kwa mujibu
wa Katiba yetu ni utoaji wa HAKI na
si USIKILIZAJI wa kesi tu. Hapo
tuelewane kabisa.
Haki ya
kusikilizwa kesi yako ina madhumuni ya
kuhakikisha kuwa unapata USAWA MBELE YA
SHERIA na si kuhakikisha unapata HAKI
mbele ya sheria. Haki inapatikana pale
Mahakama itaendeshwa na watu wenye uwezo,
uzoefu, weledi, maadili, uhuru wa fikra,
ambao hawana uoga na wanaoheshimu matakwa
ya Katiba yetu. Kusikiliza kesi na
kutoa maumuzi ni rahisi sana, na kila
mtu anaweza kufanya hivyo.
Lakini
kusikiliza kesi na kutoa maamuzi ya
haki ni vigumu maana inahitaji, KNOWLEDGE,
EXPERIENCE, INDEPENDENCE, A SENSE OF DUTY,
A CALLING AND FEARLESSNESS. Haki za
wananchi si usikilizwaji wa kesi zao tu
na haki ya kukata rufaa kwa
maana kesi inaweza kusikilizwa, kesi
inaweza kukatiwa rufaa bila ya HAKI
kutendeka. Kwa mujibu wa katiba yetu
majukumu ya Mahakama ni UTOAJI WA HAKI
KWA WAKATI.
Huwezi
ukawa mwoga na hapo hapo ukatoa Haki.
Huwezi ukaweka mbele maslahi yako na
ukatoa Haki. Utabaki na woga tu lakini Haki
(Justice) itakua ndoto. Ili tuelewe umuhimu wa
Katiba ningependa kutoa mfano mdogo tu.
Kwenye ujenzi wa Standard Gauge Railway,
vipimo baina ya vyuma vya reli vitabaki
4ft 8 ½ inch au 1,435 mm kutoka
Dar mpaka Rwanda. Hii haiwezi kubadilika hata
kama reli inapanda au kushuka mlima. Lakini
mabehewa yanaweza kubadilika.
Unaweza
kuwa na behewa la kubeba mizigo, behewa
la kubeba wanyama, behewa la kubeba mafuta,
behewa la kubeba watu daraja la
kwanza na behewa la kubeba watu daraja la
mwisho ilimradi magurudumu ya mabehewa ni
ya kutembea kwenye reli ya standard gauge.
Ukiweka behewa lenye magurudumu makubwa au
madogo kuliko ya standard gauge, behewa litapinduka
na watu watajehuriwa. Ili standard gauge
ifanye kazi ipasavyo, lazima magurudumu ya
mabehewa yote yafuate muundo wa standard gauge.
Katiba ni
reli yetu ya Standard Gauge, na kazi
ya Mahakama ni kuhakisha kwamba mabehewa yote
yanayowekwa kwenye reli yamefuata muundo wa
Standard Gauge. Siku Mahakama ikiacha
kufanya hiyo kazi kwa umakini na bila
ya uoga, watu wataathirika. Ina maana
kwamba Mahakama lazima pia ijitathmini yenyewe.
Ijiulize mara kwa mara, kweli tunafuata
Katiba ipasavyo au are we only paying
lip service to our constitution? And
if we are paying lip service who are
the beneficiaries of this lip service?
Is it the people of this country
or our own comfort? These are
hard questions to ask of oneself and
harder still is the ability to answer
these questions truthfully. A judiciary
that dismisses an allegation from the
Bar that its conduct contravenes article 107A
of the Constitution by positing “You are
using a hammer to hit a fly”
fails to understand that every constitutional
transgression is important because it does
not matter if the wheels on the wagon
for the standard gauge are 2 mm
off or 10 m off, so long as
they are off, they will not run
smoothly on the Standard Gauge. And so
it is with our country. Every
transgression of the Constitution is important
and must be checked if we are to
have a country that functions on the
rule of law and not the rule of fiat.
Sasa
nirudi kwenye ile hadithi yangu ya Shangazi.
Nikisema hiyo kesi imetokea hapa Tanzania
mtaniamini? Kwa hao mnaoniamini basi ina
maana kwamba mnaelewa udhaifu wa mfumo
wetu wa utoaji haki, na kwa wale
msioniamini, hamuelewi udhaifu huu na hamuwezi
kuubadilisha mfumo wetu kamwe, maana hamuamini. Hiyo kesi
imetokea hapa Tanzania na baada ya
miaka 15 bado iko Mahakamani. Ninangojea Mahakama
iyatafute makarabasha. The heroes of my
story are the family who still
believe in our justice system and are still
prepared to keep fighting for justice and
not merely for the right to be heard and the right of
a appeal.
Nisingependa
kumaliza bila ya kugusia uendeshaji wa
kesi za jinai Tanzania. Sisi Wanasheria
tunaona huzuni sana namna criminal justice system
inavyotumiwa kuonea na si kuendesha mashitaka
dhidi ya watuhumiwa. Watu wanakamatwa
na wanawekwa ndani bila ya dhamana wakati
upelelezi wa kesi haujakamilika. Nina maswali
mawili tu ya kuuliza: Kama upelelezi
haujakamilika unauhakika gani kwamba huyu mtu
ana kesi ya kujibu? Kama nitaendelea
na mfano wangu wa Standard Gauge,
Katiba yetu ya 1977 na mabadiliko yote
yaliyofanywa kwenye Katiba hii ni Kama
mfumo mpya wa reli. Tujiulize kweli
kukamata watu na kuwaweka ndani bila ya
haki ya dhamana ni jambo linaloweza
kuvumiliwa kwenye mfumo wa Katiba yetu
yenye Bill of Rights?
Lingekuwa
behewa, hili ni la Standard Gauge au
tumeliacha behewa lililoundwa kutembea kwenye
reli nyingine litembee kwenye reli yetu
na kila likitembea linaathiri wananchi?
Tujikumbushe kwamba non-bailable offences zilikuwepo
kwa capital offences only hata kabla
ya Katiba ya 1977 ninayoifananisha na
ujengaji wa Standard Gauge ya Katiba yetu.
Katiba
yetu imetambua haki na wajibu muhimu
wa wananchi (Bill of Rights), chakusikitisha
ni kwamba badala ya makosa yaliyokuwa
hayana dhamana kupunguzwa, yanazidi kuongezeka
kadri siku zinavyokwenda japokuwa Haki na
wajibu Muhimu wa wananchi bado unatambulika na
Katiba yetu. Tumefika mahala ambapo makosa
ya kutolipa kodi yanakuwa predicate
offences kwa makosa ya utakatishaji wa pesa
ambayo hayana dhamana. Kwa hiyo mtu
akishutumiwa kutokulipa kodi anaweza wekwa
ndani bila dhamana kwa kosa la utakatishaji
wa pesa.
Na
ataswekwa ndani mpaka pale D.P.P atakapoamua
kukamilisha upelelezi na kuendelea na kesi.
Wakati haya yanatokea, tumesahau kwamba,
huyu “mtuhumiwa” ana watoto, ana mke, ana
wazazi, ana ndugu na wote wanamtegemea
yeye. Siku D.P.P akiamua hataki
kuendelea na kesi, “mtuhumiwa” ana i tolewa bila
ya fidia. Ninajiuliza kweli hii ni
HAKI iliyodhamiriwa na Katiba yetu? Kwa
fikra zangu, Hapana, hapana na hapana tena.
Kama
nilivyosema awali kazi ya Mahakama ni
kuhakikisha Haki inatolewa kwa muda muafaka
na kwa kuzingatia misingi ya katiba hasa
Haki na Wajibu Muhimu wa wananchi.
Tusikae tukamlaumu DPP tu, maana yeye hana
wajibu wa kikatiba kutoa HAKI. Wajibu huo
ni wa Mahakama. Kwa hivyo akishitaki
watu wakati upelelezi haujakamilika, akifuta
mashitaka baada ya mtu kukaa maabusu kwa
miaka 6 akaamuru akamatwe tena pale
pale Mahakamani, tunaweza kumlaumu kwa
kutokufuata maadili ya Waendesha mashtaka, lakini
sisi sote kama wananchi, including DPP
mwenyewe, tunategemea Mahakama itende HAKI na
hakuna muhimili mwingine utakao pata lawama
isipokuwa Mahakama maana ibara 107A (1) inasema, “Mamlaka
yenye kauli ya mwisho ya utowaji haki
katika jamhuri ya muungano itakuwa ni Mahakama”.
Na wajibu huu
haukwepeki. Ninakwenda Segerea mara kwa mara
na ninataka kuwaambia, December 2018, kulikua
na watu walioko gerezani wanaume ni
1,723, kati ya hao waliofungwa kwa
mujibu ya hukumu ya Mahakama walikuwa 158
tu na walioko rumande ni 1,565. Upande
wa wanawake kulikuwa na walioko gerezani
313, waliofungwa baada ya kesi zao
kusikilizwa walikua 66 na walioko rumande
ni 247. Hiyo ndio hali halisi ya utoaji wa
HAKI kwa upande wa kesi za jinai.
Ningependa
kumalizia na ki-joke kimoja, dada yangu mpendwa
Balozi Mwanaidi Maajar anapenda kuniambia mara kwa mara. Siku
moja Tembo huko Serengeti kamuona Paa
anakimbia kweli huku akichungulia nyuma kila
baada ya hatua chache. Tembo akamsimamisha Paa
akamuuliza “Kulikoni? Mbona unakimbia kama unafukuzwa?”
Paa akamjibu huku anahema “Nasikia wanatafuta
mbuzi kwa kosa la money laundering”.
Tembo
kamtizama Paa kwa mshangao mkubwa akasema
“Sasa wewe Paa unakimbia nini? Hujijui
kwamba wewe ni Paa sio Mbuzi?”
Paa akamtizama Tembo kama vile mjinga kweli
akamjibu “Mimi ninajijua kwamba mimi ni
Paa, wewe pia unajua kwamba mimi ni
Paa, lakini hao wanaotafuta mbuzi wanajua
mimi ni Paa? Na kama hawajui
itanichukua miaka 20 kuthibitisha mahakamani kuwa
mimi ni Paa na Siyani mbuzi. Sina
muda huo”.
Alivyomaliza
kusema akaendelea kukimbia kama anakimbizwa na
ibilisi. Baada ya muda Paa akatizama
nyuma akamkuta Tembo naye anakimbia kama anafuatwa na
Israeli. Wajibu wa Wadau Sasa ninataka kusema
wajibu wa wadau. Ninachukuwa fursa hii
kuwakumbusha wananchi wajibu wao ndani ya
Ibara ya 26 inayosema kama ifuatavyo:
(1) “Kila
mtu ana wajibu wa kufuata na kuitii
Katiba hii na sheria za Jamhuri ya Muungano.
(2) “Kila mtu ana haki, kwa kufuata
utaratibu uliowekwa na sheria, kuchukua hatua
za kisheria kuhakikisha hifadhi ya Katiba
na sheria za nchi”.
Ni wajibu
wetu sote kufuata na kuitii Katiba na
kuhakikisha hifadhi ya Katiba yetu. Na
ni wajibu wetu sote kuilinda Katiba yetu
na sheria zetu. Ninataka kumaliza kwa kumnukuu
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kotoka Hotuba yake
“Nyufa” “Hatuwezi kuendelea kupuuza Katiba, ndiyo
sheria ya msingi; sheria nyingine zote
zinatokana na Katiba.
Haiwezi
kupuuzwa na hatuwezi kuendela na uatratibu
wa kupuuza Katiba ya nchi yetu au
kuwa na Rais anayeonea haya kuitetea
Katiba naye amechaguliwa kwa mujibu wa
Katiba, ameapa kuilinda Katiba hiyo halafu
anona haya hawezi kuitetea Katiba hiyo.
Mtu ambaye kawezi kuitetea Katiba ya nchi
yetu, hawezi kuilinda, hawezi kuisimamia
baada ya kiapo, hatufai. Hafai!”.
Ahsanteni.
Fatma Amani
Karume President of the Tanganyika Law Society 2018 - 2019
Dar es Salaam.
1st February
2018
----- Forwarded Message
-----
From: H. S. OTHMAN <hsothman@yahoo.com>
To: H. S. OTHMAN <hsothman@yahoo.com>
Sent: Tuesday, February 5, 2019, 4:11:13 p.m.
EST
Subject: Fatma karume
Hotuba ya Rais
wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Bibi Fatma
Amani Karume – Dar es Salaam Tarehe 06 Februari
2019.
Mheshimiwa
Dr.John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa
Prof. Ibrahim Juma, Jaji Mkuu, Mheshimiwa Spika
wa Bunge la Tanzania, Waheshimiwa Majaji wa
Mahakama ya Rufani,
Waheshimiwa
Majaji wa Mahakama Kuu, Waheshimiwa
Wasajili wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu,
Waheshimiwa
Mahakimu,
Mheshimiwa Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, Ndugu Wanasheria wasomi wenzangu,
Mabibi na
Mabwana.
Tangu
utotoni nimefundishwa kwamba vilivyokuwemo kwenye
mkoba wa mwanamke ni siri yake. Bibi,
Mama au Shangazi akikutuma kumletea mkoba
wake, kwetu ilikua marufuku kuchungulia ndani.
Leo, nitaivunja
miiko kwa kuwaeleza vichache ninavyobeba kwenye
mkoba wangu: miwani, maana sioni vizuri,
rangi ya mdomo hii ni muhimu,
kipepeo, Dar kuna joto kali, na wanaonijua
vizuri wanafahamu ukikuta pesa kwenye Mkoba
wangu ni bahati.
Lakini
sitoki bila ya kubeba Katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania. Sitaweza kugawa
kila kilichopo ndani ya mkoba isipokua
matamshi ya Katiba. Na ningependa kuanza
hotuba yangu kwa kuwakumbusha Utangulizi na
Misingi ya Katiba yetu. Katiba inaanza na
utangulizi ufuatao:
“Kwa kuwa
sisi wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati
kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi
ya UHURU, HAKI, UDUGU na AMANI: Na kwa
kuwa misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa
katika jamii yenye demokrasia ambayo serikali
yake husimamiwa na Bunge lenye wajumbe
waliochaguliwa na linalowawakilisha wananchi, na
pia yenye Mahakama huru zinazotekeleza
wajibu wa kutoa haki bila woga wala
upendeleo wowote, na hivyo kuhakikisha kwamba
haki zote za binadamu zinadumishwa na
kulindwa, na wajibu wa kila mtu unatekelezwa
kwa uaminifu.
Kwa hiyo
basi, Katiba hii imetungwa na Bunge
Maalum la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
kwa niaba ya Wananchi, kwa madhumuni ya
kujenga jamii kama hiyo, na pia kwa
ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa
na Serikali yenye kufuata misingi ya Demokrasia
na Ujamaa. “Misingi ya Katiba yetu
ni UHURU, HAKI, UDUGU, AMANI, DEMOKRASIA NA
UJAMAA.
Ni muhimu
pia kutambua kuwa neno Demokrasia limetajwa
mara mbili katika utangulizi huu. Na
waliotunga Katiba walielewa kwamba Mahakama
huru inayotoa haki bila woga wala upendeleo
wowote ina hakikisha haki zote za binadamu
zinadumishwa na kulindwa na ina umuhimu
wa pekee kwenye kulinda misingi ya katiba.
Nimeelezwa
kwamba uongozi wa Mahakama umeamua kauli
mbiu ya mwaka huu kuwa ni : “Utoaji
wa Haki kwa Wakati: Wajibu wa Mahakama na
Wadau”, na nimeambiwa nijikite kwenye mada hiyo. Nitaanza na
Wajibu wa Mahakama na nitamalizia na
wajibu wa wadau.
Wajibu wa
Mahakama.
Wajibu wa
Mahakama umewekwa wazi kwenye Katiba yetu. Ibara
107A (1) inasema, “Mamlaka yenye kauli ya
mwisho ya utowaji haki katika Jamhuri ya
Muungano itakuwa ni Mahakama”.
Ibara ya 107A(2)(b) ya
Katiba inaeleza “Katika kutoa uamuzi
wa mashauri ya madai na jinai kwa
kuzingatia sheria, Mahakama zitafuata kanuni zifuatazo,
yaani- a) Kutenda haki kwa wote bila
ya kujali Hali ya mtu, kijamii au kiuchumi;
b) kutochelewesha haki bila sababu ya kimsingi;
c) kutoa fidia ipasavyo kwa watu
wanaoathirika kutokana na makosa ya watu wengine,
na kwa mujib wa sheria mahususi
ilioyotungwa na Bunge; d) kukuza na
kuendeleza usuluhishi baina ya wanaohusika katika
migogoro. e) kutenda haki bila ya
kufungwa kupita kiasi na masharti ya
kiufundi yanayoweza kukwamisha haki kutendeka.”
Ibara 107B
“Katika kutekeleza mamlaka ya utoaji haki,
mahakama zote zitakuwa huru na zitalazimika
kuzingatia tu masharti ya Katiba na yale ya
sheria za nchi.” Kwa hiyo wajibu wa Mahakama ni kutoa
HAKI.
Hadithi hadithi………..
Hapo zamani za kale, kulikua na
familia ina baba, mama na watoto watatu,
wawili wakiume na mmoja wa kike.
Watoto wakiume wakaoa wakapata watoto.
Mtoto wa kike naye akaolewa lakini hakupata
bahati ya kuzaa. Kwa furaha kubwa
Baba na mama wakawa Babu na Bibi, na
mtoto wa kike akawa Shangazi. Muda
ukapita, Babu na Bibi wakafariki na wakaacha
mali kama mashamba na nyumba. Familia
ikakaa kikao na wakaamua msimamizi wa
mirathi awe Shangazi.
Mirathi
ikafunguliwa, na Shangazi akawa msimamizi kwa
hiyo mashamba na nyumba yakaingizwa kwenye
jina lake kama msimamizi wa mirathi, lakini
kaka zake wawili wakachukua na kuendeleza
mashamba ya vijijini naye akawa anaishi
kwenye nyumba ya Babu mjini.
Maisha
yakaendelea kama kawaida bila ya ugomvi
wowote maana familia hii ilikua ina upendo
sana. Kila wakivuna shambani kaka zake wakawa
wanamtumia mazao Shangazi mjini naye Shangazi
akawa anawasimamia kazi zao za kisheria huko mjini.
Muda ukapita, wale kaka wawili nao
wakafariki, mume wa Shangazi naye akatangulia
mbele ya haki na Shangazi akabaki
peke yake kwenye nyumba ya Babu mjini.
Siku moja
Shangazi akatuma ujumbe kijijini kwa watoto
wa kaka zake waje haraka kumuona.
Walivyosikia wito wa Shangazi, wale watoto
wakaenda mjini kumtembelea. Kufika wakamkuta
Shangazi anababaika kwa huzuni. Akawaeleza
kwamba katapeliwa. Wakamuuliza “Umetapeliwa
vipi?” Akasema “Tangu alivyofariki mume wangu
nimejisikia mpweke sana. Sasa kuna dada,
aitwaye Mtu Mwema akawa ananitembelea mara
kwa mara. Siku moja nilipokua ninaumwa akanipa
karatasi ili niweke sahihi alinilaghai kuwa
ninaweka sahihi kwenye makaratasi ili kumuwezesha
yeye anisimamie kupata matibabu. Mimi nikatia
sahihi.
Juzi
nilikua natafuta hati ya hii nyumba
na sijaiona. Naogopa Mtu Mwema
kanitapeli”. Akaanza kulia. Watoto
wakatafuta mwanasheria naye alipofanya utafiti
Wizara ya Ardhi, huyo mwanasheria akakuta
nyumba ya babu iko kwenye jina la Mtu
Mwema kwa madai kapewa na Shangazi
out of love and affection “kwa UPENDO”.
Mwanasheria msomi akatoa vitabu vyake, akatoa
sheria zake akasoma. Alivyomaliza
akawaambia watoto “Hii kesi ni rahisi sana
maana kwenye sheria yetu, kifungu cha
25(1)(a) cha Sheria ya Mikataba huwezi
kumpa mtu nyumba aliyekuwa sio ndugu yako
wa damu au ndugu wa kupitia ndoa
yako kwa UPENDO eti bila ya kulipwa
senti moja.
Mkataba
huo unakua haramu na hautokubaliwa na
Mahakama”. Akawaeleza watoto kwamba hiyo sheria
iko ili kuwalinda watu wasitapeliwe.
Watoto wakamwambia Shangazi asijali maana sheria
iko upande wake na kuna Mahakama itakayotii
na kutoa haki. Kesi ikafunguliwa ikaenda miaka
3, jaji akahamishwa. Kesi ikasimama miaka 2
maana Mahakama ikawa haina majaji wakutosha.
Miaka 5 baada ya kesi kufunguliwa ikapata
jaji mpya. Kesi ikaendelea. Baada ya miezi
michache, mara Shangazi akafariki.
Kesi
ikasitishwa tena maana sasa haiwezi kuendelea
mpaka watoto wafungue mirathi ili baada
ya kuteuliwa na mahakama msimamizi wa mirathi
ya Shangazi aendelee na kesi. Watoto
wakafungua mirathi, Mtu Mwema akapinga
mirathi akataka yeye awe msimamizi wa mirathi.
Kesi ya mirathi ikaenda miaka 5. Jaji
wa kwanza kwenye kesi ya mirathi
akahamishwa akaingia jaji mwengine.
Alivyoingia
jaji huyu Mtu Mwema akatoa pingamiza yake
ya mirathi ya Shangazi, na Mahakama
ikaamua mtoto wa kiume asimamie mirathi ya
Shangazi, huku ikamlaani sana Mtu Mwema kwa
kuchelewesha mirathi ya Shangazi pasipo sababu.
Huyu mtoto akachukua hati yake ya usimamizi
wa mirathi ya Shangazi akaenda mahakamani
ili kuendelea na kesi ya awali ya
Shangazi dhidi ya Mtu Mwema.
Kufika
Mahakamani Mtu Mwema akaweka pingamiza kusema
kama Kesi ya Shangazi itupwe kwa
sababu imechelewa sana kuendelea. Pingamizi
lake likakubaliwa na kesi ikatupiliwa mbali
baada ya miaka 17. Mtoto akaamua
kukata rufaa. Alipopewa makabrasha kutoka
Mahakamani akakuta kuna nakala za Ushahidi
hajapewa.
Alipouliza
akaambiwa na Msajili makabrasha ya Ushahidi
yamepotea. Miaka 15 ikapita bado kesi
haijakamilika, makabrasha ya Ushahidi yamepotea
mahakamani, mtoto nae kazeeka na kapata
mshtuko wa moyo. Sasa tujiulize kesi kama
hii inaweza kutokea kwenye nchi yenye
Mahakama huru zinazotekeleza wajibu wa
kutoa haki bila woga wala upendeleo na
kutochelewesha haki bila ya sababu za msingi?
Kwa maoni
yangu, na naamini mtakubaliana na mimi kuwa
kesi kama hii haiwezi kutokea kwenye
Mahakama inayotekeleza majukumu yaliyoko kwenye ibara
ya 107(A) ya Katiba yetu. Kwanza kwa sababu (1)
Mahakama yetu inatakiwa kutoa HAKI; (2)
kutochelewesha utoaji wa Haki bila ya
sababu ya kimsingi na (3) pia kutenda
haki bila kufungwa kupita kiasi na
masharti ya kiufundi yanayoweza kukwamisha haki
kutendeka. Majukumu ya Mahakama yetu
kwa mujibu wa Katiba yetu ni utoaji
wa HAKI na si USIKILIZAJI wa kesi tu.
Hapo tuelewane kabisa.
Haki ya
kusikilizwa kesi yako ina madhumuni ya
kuhakikisha kuwa unapata USAWA MBELE YA
SHERIA na si kuhakikisha unapata HAKI
mbele ya sheria. Haki inapatikana pale
Mahakama itaendeshwa na watu wenye uwezo,
uzoefu, weledi, maadili, uhuru wa fikra,
ambao hawana uoga na wanaoheshimu matakwa
ya Katiba yetu. Kusikiliza kesi na kutoa
maumuzi ni rahisi sana, na kila mtu
anaweza kufanya hivyo.
Lakini
kusikiliza kesi na kutoa maamuzi ya
haki ni vigumu maana inahitaji, KNOWLEDGE,
EXPERIENCE, INDEPENDENCE, A SENSE OF DUTY,
A CALLING AND FEARLESSNESS. Haki za wananchi
si usikilizwaji wa kesi zao tu na
haki ya kukata rufaa kwa maana kesi
inaweza kusikilizwa, kesi inaweza kukatiwa
rufaa bila ya HAKI kutendeka. Kwa
mujibu wa katiba yetu majukumu ya
Mahakama ni UTOAJI WA HAKI KWA WAKATI.
Huwezi
ukawa mwoga na hapo hapo ukatoa Haki.
Huwezi ukaweka mbele maslahi yako na
ukatoa Haki. Utabaki na woga tu lakini Haki
(Justice) itakua ndoto. Ili tuelewe umuhimu wa
Katiba ningependa kutoa mfano mdogo tu.
Kwenye ujenzi wa Standard Gauge Railway,
vipimo baina ya vyuma vya reli vitabaki
4ft 8 ½ inch au 1,435 mm kutoka
Dar mpaka Rwanda. Hii haiwezi kubadilika hata
kama reli inapanda au kushuka mlima. Lakini
mabehewa yanaweza kubadilika.
Unaweza
kuwa na behewa la kubeba mizigo, behewa
la kubeba wanyama, behewa la kubeba mafuta,
behewa la kubeba watu daraja la
kwanza na behewa la kubeba watu daraja la
mwisho ilimradi magurudumu ya mabehewa ni
ya kutembea kwenye reli ya standard gauge.
Ukiweka behewa lenye magurudumu makubwa au
madogo kuliko ya standard gauge, behewa
litapinduka na watu watajehuriwa. Ili
standard gauge ifanye kazi ipasavyo, lazima
magurudumu ya mabehewa yote yafuate muundo wa
standard gauge.
Katiba ni
reli yetu ya Standard Gauge, na kazi
ya Mahakama ni kuhakisha kwamba mabehewa
yote yanayowekwa kwenye reli yamefuata muundo
wa Standard Gauge. Siku Mahakama ikiacha
kufanya hiyo kazi kwa umakini na bila
ya uoga, watu wataathirika. Ina maana
kwamba Mahakama lazima pia ijitathmini yenyewe.
Ijiulize mara kwa mara, kweli tunafuata
Katiba ipasavyo au are we only paying
lip service to our constitution? And
if we are paying lip service who are
the beneficiaries of this lip service?
Is it the people of this country
or our own comfort? These are
hard questions to ask of oneself and
harder still is the ability to answer
these questions truthfully. A judiciary
that dismisses an allegation from the
Bar that its conduct contravenes article
107A of the Constitution by positing “You
are using a hammer to hit a
fly” fails to understand that every
constitutional transgression is important because
it does not matter if the wheels on
the wagon for the standard gauge are
2 mm off or 10 m off, so long
as they are off, they will not
run smoothly on the Standard Gauge.
And so it is with our country.
Every transgression of the Constitution is important
and must be checked if we are to
have a country that functions on the
rule of law and not the rule of fiat.
Sasa
nirudi kwenye ile hadithi yangu ya Shangazi.
Nikisema hiyo kesi imetokea hapa Tanzania
mtaniamini? Kwa hao mnaoniamini basi ina
maana kwamba mnaelewa udhaifu wa mfumo
wetu wa utoaji haki, na kwa wale
msioniamini, hamuelewi udhaifu huu na hamuwezi
kuubadilisha mfumo wetu kamwe, maana hamuamini. Hiyo kesi
imetokea hapa Tanzania na baada ya
miaka 15 bado iko Mahakamani. Ninangojea Mahakama
iyatafute makarabasha. The heroes of my
story are the family who still believe
in our justice system and are still
prepared to keep fighting for justice and
not merely for the right to be heard and the right of
a appeal.
Nisingependa
kumaliza bila ya kugusia uendeshaji wa
kesi za jinai Tanzania. Sisi Wanasheria
tunaona huzuni sana namna criminal justice system
inavyotumiwa kuonea na si kuendesha mashitaka
dhidi ya watuhumiwa. Watu wanakamatwa
na wanawekwa ndani bila ya dhamana wakati
upelelezi wa kesi haujakamilika. Nina maswali
mawili tu ya kuuliza: Kama upelelezi
haujakamilika unauhakika gani kwamba huyu mtu
ana kesi ya kujibu? Kama nitaendelea
na mfano wangu wa Standard Gauge,
Katiba yetu ya 1977 na mabadiliko yote
yaliyofanywa kwenye Katiba hii ni Kama
mfumo mpya wa reli. Tujiulize kweli
kukamata watu na kuwaweka ndani bila ya
haki ya dhamana ni jambo linaloweza
kuvumiliwa kwenye mfumo wa Katiba yetu
yenye Bill of Rights?
Lingekuwa
behewa, hili ni la Standard Gauge au
tumeliacha behewa lililoundwa kutembea kwenye
reli nyingine litembee kwenye reli yetu
na kila likitembea linaathiri wananchi?
Tujikumbushe kwamba non-bailable offences zilikuwepo
kwa capital offences only hata kabla ya
Katiba ya 1977 ninayoifananisha na ujengaji
wa Standard Gauge ya Katiba yetu.
Katiba
yetu imetambua haki na wajibu muhimu
wa wananchi (Bill of Rights), chakusikitisha
ni kwamba badala ya makosa yaliyokuwa
hayana dhamana kupunguzwa, yanazidi kuongezeka
kadri siku zinavyokwenda japokuwa Haki na
wajibu Muhimu wa wananchi bado unatambulika
na Katiba yetu. Tumefika mahala ambapo
makosa ya kutolipa kodi yanakuwa predicate
offences kwa makosa ya utakatishaji wa pesa
ambayo hayana dhamana. Kwa hiyo mtu
akishutumiwa kutokulipa kodi anaweza wekwa
ndani bila dhamana kwa kosa la utakatishaji
wa pesa.
Na
ataswekwa ndani mpaka pale D.P.P atakapoamua
kukamilisha upelelezi na kuendelea na kesi.
Wakati haya yanatokea, tumesahau kwamba,
huyu “mtuhumiwa” ana watoto, ana mke, ana
wazazi, ana ndugu na wote wanamtegemea
yeye. Siku D.P.P akiamua hataki
kuendelea na kesi, “mtuhumiwa” ana i tolewa bila
ya fidia. Ninajiuliza kweli hii ni
HAKI iliyodhamiriwa na Katiba yetu? Kwa
fikra zangu, Hapana, hapana na hapana tena.
Kama
nilivyosema awali kazi ya Mahakama ni
kuhakikisha Haki inatolewa kwa muda muafaka
na kwa kuzingatia misingi ya katiba hasa
Haki na Wajibu Muhimu wa wananchi.
Tusikae tukamlaumu DPP tu, maana yeye hana
wajibu wa kikatiba kutoa HAKI. Wajibu huo
ni wa Mahakama. Kwa hivyo akishitaki
watu wakati upelelezi haujakamilika, akifuta
mashitaka baada ya mtu kukaa maabusu kwa
miaka 6 akaamuru akamatwe tena pale
pale Mahakamani, tunaweza kumlaumu kwa
kutokufuata maadili ya Waendesha mashtaka, lakini
sisi sote kama wananchi, including DPP
mwenyewe, tunategemea Mahakama itende HAKI na
hakuna muhimili mwingine utakao pata lawama
isipokuwa Mahakama maana ibara 107A (1) inasema, “Mamlaka
yenye kauli ya mwisho ya utowaji haki
katika jamhuri ya muungano itakuwa ni Mahakama”.
Na wajibu huu
haukwepeki. Ninakwenda Segerea mara kwa mara
na ninataka kuwaambia, December 2018, kulikua
na watu walioko gerezani wanaume ni
1,723, kati ya hao waliofungwa kwa
mujibu ya hukumu ya Mahakama walikuwa 158
tu na walioko rumande ni 1,565.
Upande wa wanawake kulikuwa na walioko gerezani
313, waliofungwa baada ya kesi zao
kusikilizwa walikua 66 na walioko rumande
ni 247. Hiyo ndio hali halisi ya utoaji wa
HAKI kwa upande wa kesi za jinai.
Ningependa
kumalizia na ki-joke kimoja, dada yangu mpendwa
Balozi Mwanaidi Maajar anapenda kuniambia mara kwa mara. Siku
moja Tembo huko Serengeti kamuona Paa
anakimbia kweli huku akichungulia nyuma kila
baada ya hatua chache. Tembo akamsimamisha Paa
akamuuliza “Kulikoni? Mbona unakimbia kama unafukuzwa?”
Paa akamjibu huku anahema “Nasikia wanatafuta
mbuzi kwa kosa la money laundering”.
Tembo
kamtizama Paa kwa mshangao mkubwa akasema
“Sasa wewe Paa unakimbia nini? Hujijui
kwamba wewe ni Paa sio Mbuzi?”
Paa akamtizama Tembo kama vile mjinga kweli
akamjibu “Mimi ninajijua kwamba mimi ni
Paa, wewe pia unajua kwamba mimi ni
Paa, lakini hao wanaotafuta mbuzi wanajua
mimi ni Paa? Na kama hawajui
itanichukua miaka 20 kuthibitisha mahakamani kuwa
mimi ni Paa na Siyani mbuzi. Sina
muda huo”.
Alivyomaliza
kusema akaendelea kukimbia kama anakimbizwa na
ibilisi. Baada ya muda Paa akatizama
nyuma akamkuta Tembo naye anakimbia kama anafuatwa na Israeli.
Wajibu wa Wadau Sasa ninataka kusema wajibu
wa wadau. Ninachukuwa fursa hii kuwakumbusha
wananchi wajibu wao ndani ya Ibara ya
26 inayosema kama ifuatavyo:
(1) “Kila
mtu ana wajibu wa kufuata na kuitii
Katiba hii na sheria za Jamhuri ya Muungano.
(2) “Kila mtu ana haki, kwa
kufuata utaratibu uliowekwa na sheria, kuchukua
hatua za kisheria kuhakikisha hifadhi ya
Katiba na sheria za nchi”.
Ni wajibu
wetu sote kufuata na kuitii Katiba na
kuhakikisha hifadhi ya Katiba yetu. Na
ni wajibu wetu sote kuilinda Katiba
yetu na sheria zetu. Ninataka kumaliza kwa
kumnukuu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kotoka
Hotuba yake “Nyufa” “Hatuwezi kuendelea kupuuza
Katiba, ndiyo sheria ya msingi; sheria
nyingine zote zinatokana na Katiba.
Haiwezi
kupuuzwa na hatuwezi kuendela na uatratibu
wa kupuuza Katiba ya nchi yetu au
kuwa na Rais anayeonea haya kuitetea
Katiba naye amechaguliwa kwa mujibu wa
Katiba, ameapa kuilinda Katiba hiyo halafu
anona haya hawezi kuitetea Katiba hiyo.
Mtu ambaye kawezi kuitetea Katiba ya nchi
yetu, hawezi kuilinda, hawezi kuisimamia
baada ya kiapo, hatufai. Hafai!”.
Ahsanteni.
Fatma Amani
Karume President of the Tanganyika Law Society 2018 - 2019
Dar es Salaam.
1st February
2018
No comments :
Post a Comment