Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, February 5, 2019

Msimamo wa serikali juu ya mashamba ya Mo Dewji!

Serikali imesema mashamba sita yanayomilikiwa na Mohamed Dewji ambaye ni mfanyabiashara maarufu yapo chini ya uangalizi na iwapo atashindwa kutekeleza masharti watayafuta.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati akijibu hoja za wabunge walizozitoa katika mjadala wa taarifa ya kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii.

Lukuvi amesema awali mfanyabiashara huyo alipewa onyo katika mashamba 12 kati ya 21 aliyokuwa akimiliki.

Aidha amesema Serikali tayari imefuta hati za mashamba sita bado sita ambayo yapo kwenye uangalizi na kubainisha kuwa Tanzania ina mashamba makubwa 2000 ya kilimo na ufugaji.

Lukuvi amesema kwa kipindi cha miaka mitatu wamefuta mashamba 46 katika maeneo mbalimbali ambayo yameshindwa kutimiza masharti.


No comments :

Post a Comment