Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Mhe. Freeman Mbowe ambaye bado yuko mahabusu Gereza la Segerea pamoja na Mbunge Esther Matiko, amemtumia salaam za pole na kumtakia uponaji wa haraka Mzee Sumaye ili arejee katika majukumu yake.
Aidha, Katibu Mkuu wa Chama, Dkt. Vincent Mashinji, Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA Patrick Ole Sosopi pamoja na viongozi wengine wa Chama hicho ngazi na maeneo mbalimbali ya nchi, wamefika hospitalini hapo kumjulia hali na kumpatia pole Mzee Sumaye ambaye pia Mwenyekiti wa Chama Kanda ya Pwani.
No comments :
Post a Comment