Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, February 11, 2019

RAIS DKT. SHEIN AJUMUIKA NA ASKARI WA VIKOSI VYA ULINZI NA USALAMA WALIOSHIRIKI GWARIDE LA MIAKA 55 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR!


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Kaimu Kamanda wa Brigedi ya 101KV Zanzibar Kanali.S.S.Mugoba, alipowasili katika viwanja vya Kambi ya Chukwani Zanzibar kujumuika na Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama walioshiriki Gwaride la Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba mwaka huu 2019.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, akiwa amesimama wakati ukipigwa wimbo wa Taifa baada ya kuwasili katika viwanja vya Kambi ya JWTZ Chukwani Zanzibar, kujumuika na Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama walioshiriki Gwaride la Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, kushoto Kaimu Kamanda wa Brigedi ya 101KV Zanzibar Kanali S.S.Mugoba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Gavu na kulia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mikoa na Idara Maalum za SMZ.Mhe. Haji Omar Kheri.(Picha na Ikulu) 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa amesimama, ukipigwa wimbo wa Taifa baada ya kuwasili katika Viwanja vya Kambi ya Chukwani kujumuika na Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama kujumuika katika chakula maalum aliowaandalia kushoto Kaimu Kamanda wa Brigedi ya 101KV Zanzibar, Kanali S.S.Mugoba na kulia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ. Mhe. Haji Omar Kheri,(Picha na Ikulu)
KAIMU Kamanda Brigedi ya 101 KV Zanzibar Kanali S.S.Mugoba, akizungumza wakati wa hafla ya chakula maalum kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Aki Mohamed Shein, kwa ajili ya Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama walioshiriki gwaride la Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi zilizofanyika mwaka huu kisiwani Pemba January,12, 2019.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein, akijumuika katika chakula maalum aliowaandalia, Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama, katika kambi ya chukwani walioshiriki Gwaride la Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi Zanzibar mwaka huu zilizofanyika Kisiwani Pemba katika uwanja wa gombani.
ASKARI wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama walioshiriki Gwaride la Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 55 ya Mapinduzi Zanzibar, wakijumuika katika hafla ya chakula maalum walioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, hafla hiyo imefanyika katika Kambi ya Chukwani Zanzibar.
ASKARI wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama wakijumuika katika hafla ya chakula maalum kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Kambi ya Chukwani Zanzibar.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gavu akitowa shukrani kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Kambi ya Chukwani Zanzibar.
ASKARI wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama wakifuatilia hutuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gavu akitowa shukrani kwa niaba ya Rais wa Zanzibar, wakati wa hafla ya chakula maalum kilichoandaliwa kwa ajili yao katika kambi ya Chukwani Zanzibar.(Picha na Ikulu)

No comments :

Post a Comment