Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, March 21, 2019

ACT Wazalendo Zanzibar wamkaribisha Maalim Seif!


Na. Thabit hamidu, Zanzibar
Katibu Msaidizi kamati ya Itikadi na uenezi Chama cha ACT Wazalendo upande wa Zanzibar Seif Hamadi Suleimani amesema hatua alioichukua Maalim Seif kuhamia Chama cha ACT Wazelendo ni mwanzo mwema wa kudai haki nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari  katika Ofisi Kuu za Chama hicho zilizopo kidongo Chekundu Mjini maghari Unguja katibu huyo alisema kitendo alikifanya Maalim Seif kinaonesha ukomavu wa siasa na mwanzo mwema wa mapambano dhidi ya kudai haki Nchini.

"Uamuzi wa kuhamia ACT kwa maalim Seif imeweka historia mpya katika siasa za Tanzania hivyo kama ACT Wazalendo tunamkaribisha katika chama chetu," Alisema katibu wa Uwezi ACT Zanzibar.

Aidha alichua fursa hiyo kumkaribisha Maalim Seif Sharif Hamadi katika chama hicho na kuwa huru na haki kama wanachama wengine ndani ya chama hicho.

"Nichukue fursa hii kumkaribisha maalim katika chama chetu yeye na viongozi waliongia toka tarehe 18 na wajisikie huru ambapo wanahaki kama wanachama wengine waliowakuta ndani ya chama hichi," aliongeza kusema.

Machi 18 mwaka huu aliekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha wanachi CUF na Muasisi wa Chama hicho alichukua uamuzi wa kuhama chama na kuhamia ACT kutokana na mgogoro uliokuwa unaendelea ndani ya chama chake.

No comments :

Post a Comment