Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, March 22, 2019

CUF Zanzibar kufanya ziara ya kukagua ofisi zake!


Makamu mwenyekiti wa CUF Zanzibar,  Abass Juma Muhunzi amesema chama hicho kitafanya ziara katika ofisi zake zote Zanzibar baada ya kumalizika kile alichokiita ‘vurugu’ alizodai kufanywa na wanachama wa chama cha ACT-Wazalendo.

Ametoa kauli hiyo leo, katika mkutano wake na waandishi wa habari kuzungumzia vitendo vya ofisi za CUF kubadilishwa kuwa na ACT, baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad kujiunga na ACT.

Amesema licha ya kuwa na mpango wa kuyatembea matawi hayo ili kupanga mikakati kichama, lakini wakati huu hawawezi kufanya hivyo kutokana na wanachama wa ACT kupaka rangi za chama hicho ofisi za CUF.

"Kitendo cha kuyapaka rangi za ACT matawi yetu hakuna maana kwamba si ya kwetu. Bado  tunayatambua na muda ukifika wa kuyatembelea tutafanya hivyo"alisema.

“Tunafahamu watatutia hasara ya kuyabadili rangi matawi yetu, lakini haitajalisha kitu kwani tunajua wanachofanya bado hawakielewi.”

No comments :

Post a Comment