Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ Juma Ameir Hafidh.
Mara baada ya BOT kufungia vituo vya kuuzia na kunulia pesa za kigeni,Benk ya watu wa Zanzibar PBZ kesho rasmi wanaanza kutoa huduma hiyo mara baada ya kupatiwa leseni na BOT.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Mkurugenzi Mtendaji wa Benk ya watu wa Zanzibar PBZ Juma Ameir hafidhi alisema PBZ wamepatiwa leseni ya kuendesha biashara hiyo mara baada ya kukidhi vigezo vinavyotaiwa katika uendeshaji wa biashara hiyo.
Alisema Moja kigezo ni kuwa na mfumo ambao hautaruhusu uingizaji wa pesa haramu katika mifumo ya kifedha.
Aidha alisema hapo awali Benk ya watu wa Zanzibar PBZ walikuwa wanatoa huduma hiyo ya kuuza na kununua pesa za kigeni kwa wateja wa benki hiyo tu tofauti na hivi sasa ambapo wamepatiwa leseni ya kutoa huduma hiyo kwa wananchi wote.
"Leseni hii kina maanisha kuwa PBZ wataendesha huduma ya kununua na kuuza fedha za kigeni kwa wananchi wote bila ya kujali ni mteja wa benk gani”alieleza Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ.
Aidha alisema tayari wameshajipanga katika uendeshaji wa biashara hiyo ambapo wameshawapatia mafunzo maalumu wafanyakazi wa benki katika uendeshaji wa biashara hiyo.
Hata hivyo alisema huduma hiyo itatolewa katika matawi yote ya PBZ unguja na Pemba na vituo vipya vilivyoanzishwa kwa ajili ya utoaji wa huduma hiyo.
"Matawi yetu yote ya PBZ tutatoa huduma hiyo pamoja na vituo kadhaa ambavyo tumvianzisha kama vile darajani na maeneo mengine ya utoaji wa huduma hii” alisema Mkurugenzi.
Aidha alisema wanampango wa kuongeza vituo vingine kwa ajili ya kutoa huduma hiyo kulingana na mahitaji yatayohitajika.

No comments :
Post a Comment