Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, March 4, 2019

PROFESA KABUDI APEWA SOMO NA MHE TUNDU LISSU JUU YA SHERIA ZA NCHI YETU!!!

PROF. KABUDI AANZA KAZI KWA VITISHO!

MWNAHARAKATI MHE. TUNDU LISSU!

PROFESA WETU WA SHERIA HAJUI SHERIA ZETU???

Tundu AM Lissu, MP 
Tienen, Ubelgiji 

Nimemsikia Waziri wetu mpya wa Mambo ya Nje, Profesa Palamagamba Kabudi akifokea na kutishia watu anaodai wanaisema vibaya na 'kuibagaza' nchi yetu.

Profesa Kabudi anatakiwa afahamu kwamba Watanzania sio tena watu wa kufokewa na kutishiwa kama watoto wa shule wa zamani.

Pili, kwa vile ni profesa wa sheria anayeelekea kutokufahamu au kuamini matakwa ya Katiba na Sheria za nchi yetu, nawaombeni mmwambie Profesa Kabudi mambo yafuatayo:

1. Kwamba, kwa mujibu wa Katiba yetu, kuna tofauti kubwa kati ya 'nchi' na 'Serikali.'

(a) 'Nchi' ya Tanzania ni ile inayotamkwa kwenye ibara ya 1 na 2(1) ya Katiba kuwa "... ni Jamhuri ya Muungano (inayojumuisha) ... eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo."


(b) Kwa upande mwingine, 'Serikali' ya Tanzania imefafanuliwa katika ibara ya 6 ya Katiba kuwa "... ni pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Serikali za mitaa na pia mtu anayetekeleza madaraka au mamlaka yoyote kwa niaba ya Serikali yoyote."

(c) Matendo maovu ya vyombo vya usalama kama Jeshi la Polisi au Idara ya Usalama wa Taifa na Ujasusi; au ya viongozi wa serikali kama Rais, Mawaziri au Wakuu wa Mikoa na Wilaya; au watendaji wake wengine, sio matendo ya 'nchi' bali ni matendo ya 'Serikali.'

Matendo haya ya 'Serikali' yanaweza yakapingwa, kubezwa, kubagazwa, kusemwa vibaya au kuchafuliwa bila kuichafua au kuibeza au kuibagaza 'Nchi.'

2. Kwamba kuisema Serikali vibaya, au kuibagaza, au kuichafua - ndani au nje ya nchi - kwa sababu ya matendo yake maovu - sio kosa bali ni wajibu wa kila mtu na hasa kila raia wa Tanzania.

(a) Kwa mujibu wa ibara ya 3(1) ya Katiba yetu, Tanzania "... ni nchi ya kidemokrasia ... yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa." Nchi yetu sio ya Chama kimoja kama ilivyokuwa zamani, kwa hiyo kuipinga au kuikosoa Serikali iliyoko madarakani sio kosa, bali ni kutekeleza matakwa ya Katiba.

(b) Kwa mujibu wa ibara ya 8(1)(a) "... wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi...."

Aidha, ibara ya 8(1)(c) inasisitiza kwamba "Serikali itawajibika kwa wananchi." Kwa maana hiyo, sisi wananchi ndio tuko juu ya Serikali. 


Kuipinga, kuisema vibaya, kuibagaza au kuichafua Serikali hiyo kutokana na matendo yake maovu, hakuwezi kuwa kosa hata kidogo, bali ni sehemu ya kuiwajibisha kwetu.

3. Mwambieni Profesa Kabudi kwamba Serikali yetu ina wajibu mbele ya jumuiya ya kimataifa wa kuheshimu haki za binadamu zilizoainishwa kwenye Katiba yetu.

(a) Ibara ya 9(f) ya Katiba inaitaka "... Mamlaka ya Nchi na vyombo vyake vyote ... kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha ... kwamba heshima ya binadamu inahifadhiwa na kudumishwa kwa kufuata Kanuni za Tangazo la Dunia kuhusu Haki za Binadamu."

(b) Serikali yetu imesaini mikataba mbali mbali ya kimataifa na ya kikanda inayotulazimu kuheshimu haki za binadamu za wananchi wetu.

(c) Serikali yetu imekubali, kwa kusaini Mkataba wa Roma unaounda Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, kwamba itawajibika kwa jumuiya ya kimataifa kwa vitendo vyovyote vya ukiukwaji wa haki za binadamu vilivyokatazwa na Mkataba wa Roma.

(d) Kama sehemu ya uwajibikaji wetu mbele ya jumuiya ya kimataifa kuhusu masuala ya haki za binadamu, Serikali yetu inatakiwa kupeleka taarifa ya utekelezaji wa wajibu wake huo kwenye vyombo vya uwajibikaji vya kimataifa, kama vile Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa. Hivi ndivyo alivyofanya Profesa Kabudi mwenyewe wiki iliyopita kule Geneva, Uswisi.

No comments :

Post a Comment