Na Thabit Madai.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema haitaacha kuchukua hatua kali kwa Wafanyabiashara watakao ingiza bidhaa isiyokuwa na kiwango kwa ajili ya matumizi ya wananchi.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda Hassan Khamis Hafidh wakati alipofika bandari ya Malindi kuangalia zoezi la kuhamisha tan 520 za sukari kwenda kuangamizwa.
Ambapo bidhaa hizo zinaangamizwa kwenye mashimo ya mchanga katika kijiji cha zingwezingwe baada ya kukosa kiwango kwa matumizi ya bianadamu.
Naibu waziri alisema kuwa Serikali ipo makini kulinda afya za Wananchi wake hivyo haitakubali kuingizwa bidhaa yoyote isiyofaa kwa matumizi ya wananchi ili kuwaepusha na maradhi.
Aidha alisema ulinzi mkali wa vikosi vya ulinzi na usalama umeandaliwa kwa ajili ya kusimamia sukari hiyo ili kuhakikisha hakuna mtu atakaefanya mbinu ya kuipata mpaka zoezi zima la kuiangamiza limalizike.
Aliwataka Wafanyabiashara kuendesha biashara zao kwa njia za halali na kuacha tabia ya kununua bidhaa za gharama nafuu bila ya kuangali ubora wake kwa lengo la kutafuta faida kubwa.
Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************


No comments :
Post a Comment