Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa CUF, amekabidhiwa kadi namba moja ya Chama cha ACT Wazalendo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Dar es Salaam amesema ameamua kuhamia ACT Wazalendo kuanzisha vuguvugu la kuking'oa chama cha Mapinduzi.
"Waandishi na baadhi ya wanachama wananiuliza kwanini nimehamia kwenye chama kidogo ninewaambia wakati tunaanzisha vuguvugu la kuking'oa chama cha Mapinduzi hatukuhitaji mtu mwenye nguvu bali tulihitaji chama cha siasa chochote,hiki ni chama chenye malengo na nia ya kufika mbali nitaendelea na vuguvugu kutokea hapa" amesema Maalim Seif.
Baadhi ya Wanachama wengine wa CUF waliokabidhiwa Kadi za ACT Wazalendo, ni pamoja na aliyekuwa Mgombea mwenza wa Urais katika Uchaguzi wa mwaka 2015 kwa tiketi ya CHADEMA, Juma Duni Haji, na Ismail Jussa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Dar es Salaam amesema ameamua kuhamia ACT Wazalendo kuanzisha vuguvugu la kuking'oa chama cha Mapinduzi.
"Waandishi na baadhi ya wanachama wananiuliza kwanini nimehamia kwenye chama kidogo ninewaambia wakati tunaanzisha vuguvugu la kuking'oa chama cha Mapinduzi hatukuhitaji mtu mwenye nguvu bali tulihitaji chama cha siasa chochote,hiki ni chama chenye malengo na nia ya kufika mbali nitaendelea na vuguvugu kutokea hapa" amesema Maalim Seif.
Hata hivyo amewata wanachama wenzake wa ACT kutojibizana kwenye mitandao kwani kwa kufanya hivyo watawapa nafasi washindani wao, Maalim amewataka wanachama kutumia muda wao kukijenga chama kwani nguvu ya chama ni Watu.

No comments :
Post a Comment