dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, March 21, 2019

Waziri Mkuu New Zealand ataka hatua za kimataifa kuhusu mitandao ya kijamii!


Waziri Mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua ya kuikabili hatari inayosababishwa na mitandao ya kijamii.

Kiongozi huyo ametowa mwito huu wakati jamii ya Waislamu nchini humo ikianza kuwazika wapendwa wao waliouawa siku tano zilizopita katika mashambulizi kwenye misikiti miwili.

Mshambuliaji anayeamini kwamba watu weupe ni bora zaidi, alionesha tukio la mauaji hayo moja kwa moja kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook kwa dakika 17.

 Anatuhumiwa kwa kuwauwa waumini 50 wa Kiislamu wakati wa sala yao ya Ijumaa. Facebook ilisema chini ya watu 200 walitazama video hiyo moja kwa moja, lakini ililazimika kuondoa video milioni 1.5 zilizosambazwa kuhusu mauaji hayo ya kinyama.


Ardern amesema kwamba wakati lengo lake liko kwa watu wa New Zealand, yapo masuala ambayo viongozi wa ulimwengu wanapaswa kuyakabili kwa pamoja. Anasema mitandao ya kijamii haipaswi kuendelea kutumiwa kama majukwaa ya kueneza chuki na kusababisha machafuko.

No comments :

Post a Comment