Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, March 21, 2019

Waziri wa Afya Zanzibar awashauri watafiti kufanya tafiti za kinywa na meno!


Waziri wa Afya Zanzibar,  Hamad Rashid Mohammed amewashauri wataalamu wa afya nchini kufanya utafiri ili kujua kiwango cha maradhi ya kinywa na meno na matibabu yake.
Akizungumza katika kilele cha siku ya Maadhimisho ya Kinywa na meno ambapo Zanzibar yamefanyika katika viwanja vya Mnara wa Kisonge mjini magharib Unguja.

Waziri hamadi Amesema utafiti huo utaweza kusaidia kutoa taaluma zaidi kwa Walimu wanaofundisha watoto wakiwa skuli na hivyo kuwajengea uwezo wa kujikinga na matatizo ya kutoboka kwa meno na kuvimba fizi.


Amefahamisha kuwa kufanyika kwa utafiti huo kutasaidia kupatikana kwa takwimu sahihi na kuweza kujua ukubwa wa maradhi hayo na kupatiwa ufumbuzi wake.

Aidha amewataka wananchi kuvitumia Vituo vya afya na hospitali za serikali kupata huduma zilizobora ili kuondoa matatizo yanayowakabili.

“Nia ya Serikali ni kuwa na taifa la watu wenye afya ni vyema kupima afya zetu angalau mara mbili kwa mwaka katika Vituo vya afya vilivyokaribu nasi,” alieleza Wazri Hamad

Aidha Waziri huyo wa Afya aliwaomba wananchi kufanya usafi wa kinywa pamoja na kuwafundisha watoto namna ya kupiga mswaki ili kuepuka matatizo kutoboka kwa meno na kutoa harufu katika kinywa.

“Asilimia 90 ya matibabu ya maradhi haya tunayo wenyewe, tiba zaidi ni kuwa wasafi, hivyo nawaomba sana kuzingatia usafi maana afya ni usafi” alisisitiza Waziri Hamad.

No comments :

Post a Comment