Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe amesema kuwa Chama cha ACT Wazalendo hakina ugomvi aina yoyote na dola ila wao wanaendeleza harakati ukombozi Nchini.
Amesema kwa muda mrefu wananchi Nchini wamekuwa wakikosa kupata haki zao za msingi hivyo uwepo wa chama hicho ni fursa ya kuwapatia wanachi hao haki zao za msingi.
Hayo aliyabainisha leo katika Ukumbi wa Chama cha ACT zilizopo Vuga mara baada ya kuwasili Zanzibar akifuatana na mwenyeji wake Maalim Seif Sharif Hamadi.
Zito Amesema azma ya chama hicho ni kutetea wananchi walio wanyonge kwa kuwapatia haki zao za kidemokrasia,haki ya kufanya siasa pamoja na haki ya kukosoa pale panapopaswa kukosolewa.
“kutokana na mazingira yaluyopo sasa ya Tanzania haki zote zimeminywa na kumpelekea Maalimu seif sharif aliyekuwa katibu wa CUF pamoja na wafuasi wake kujiunga na chama cha ACT”alisema Zito.
Aidha Zitto amedai kuwa sababu ya waliokuwa wafuasi wa CUF kuhamia chama hicho kutokana na ukandamizaji huo ambao unafanywa dhidi ya haki za watu kufanya siasa na kutetea haki.
Hata hivyo amesema bado wananchi wa Tanzania wanaendelea kuburuzwa na kukoseshwa haki zao kidemokrasia hasa upande wa Zanzibar katika sehemu ya muungano ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikikandamizwa kutoweza kufanyausawa wa haki hivyo watahakikisha wanalitafutia ufumbuzi wake.
Akizungumzia suala la huduma za maendeleo amesema miongoni mwa mikakati iliyopangwa katika chama cha ACT Wazalendo ni kuimarisha huduma za maji safi na salama,kuimarishwa huduma za matibabu,elimu bora kwa wananchi ili kuhakikisha muungano haumkandamizi mtu.
Amesema mbali na hayo lakini bado wafanyabiashara wanakandamizwa hasa katika utoaji wa kodi kubwa pindi wanaposafirisha biashara zao jambo ambalo linapelekea wafanyabiashara kushindwa kupata maendeleo.

No comments :
Post a Comment