Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, May 4, 2019

Amref yazindua Mradi wa afya kamilifu Zanzibar!

Shirika la Amref Health Afrika limezindua  mradi wa afya kamili wenye lengo la kupanua huduma za matunzo na matibabu ya kufubaza virusi vya ukimwi ndani ya visiwani Zanzibar. Mradi huo umezinduliwa katika Hotel Verde iliyopo Mtoni Marine Mjini Magharib Unguja na kuhudhuriwa na wadau mbali mbali wa sekta ya Afya Nchini.

Akizungumza katika Uzinduzi wa Mradi huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar amesema licha ya Zanzibar kuwa chini ya aAsilimia moja ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi bado jitihada zinahitajika kuchukuliwa katika kupamabana na maradhi hayo.
Alisema hali ya maambukizi ya virusi vya ukimwi Zanzibar bado inaridhisha lakini watafiti wamegundua kuwa makundi maalumu bado yana hitaji msaada na maangalizi ya kutosha kutokana na kuwa na idadi kubwa ya maasmbukizi ya Ugonjwa huo.

“Makundi kama vile watumiaji wa dawa za kulevya na wale wanaofanya mapenzi ya jinsia moja maambukizi kwao yamekuwa yakiongezeka maradufu,”alisema katibu Mkuu.

"Hivyo kupitia mradi huu makundi hayo yatafikiwa kwa kupatiwa elimu na huduma za matibabu ya kufubaza virusi vya Ukimwi kwa wale ambao wameshapata maambukizi," ameeleza.

Nae Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Amref Health Afrika. Dkt. Florence Temu alisema Mradi huo unalenga kuongeza idadi ya watu wanaojijua kuwa wanaishi na virusi vya Ukimwi na kupata huduma za matibabu na ushauri kwa Zanzibar.

No comments :

Post a Comment