Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, May 20, 2019

Baraza la kijeshi Sudan larejea mazungumzo na waandamanaji!

Baraza la kijeshi linaloongoza nchini Sudan linakutana na waandamanaji hii leo kujadilia kipindi cha mpito wa kisiasa baada ya mazungumzo hayo kusitishwa kwa siku tatu huku barabara zikisafishwa nje ya eneo kuu walikokusanyika waandamanaji katika mji mkuu wa Khartoum.

Pande hizo mbili zimeshiriki duru kadhaa za mazungumzo tangu jeshi la nchi hiyo lilipoipindua Serikali ya Rais Omar al-Bashir mwezi uliopita baada ya miezi minne ya maandamano makubwa dhidi ya utawala wake.

Hapo jana, Naibu mkuu wa baraza hilo la kijeshi Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo alisema maafisa usalama wamewakamata wahusika wa mashambulizi dhidi ya waandamanaji wiki iliyopita yaliosababisha vifo vya watu watano ikiwa ni pamoja na afisa mmoja wa kijeshi.
Wanajeshi na waandamanaji hao walisema kuwa mashambulizi hayo yalitekelezwa na wafuasi wa al- Bashir.

Wakati huo huo Saudi Arabia imefahamisha kuwa imeweka dola milioni 250 kwenye benki kuu ya Sudan, kuimarisha hali ya kifedha ya nchi hiyo na kuipunguzia shinikizo sarafu ya pauni ya sudan. Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu kutoa msaada wa dola bilioni 3 kwa nchi hiyo baada ya kuondolewa kwa rais Bashir.

No comments :

Post a Comment