Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, May 3, 2019

ZITTO KABWE ON THE ECONOMY OF TANZANIA!

Nimemsikia Rais akisema pale Mbeya kuwa Uchumi wetu bado unakua kwa 7%. Pia nimeona Jeshi la Watetezi wa mambo ya hovyo wakiongozwa na Bwana Mwigulu Nchemba wakirudia maneno hayo kama kasuku bila kujua kuwa IMF Ndio mamlaka pekee ya Dunia ya masuala ya ‘ economic surveillance’. ‬

‪IMF wamesema wazi kabisa kuwa “ kama Sera  za kiuchumi za Tanzania hazitatazamwa upya na kuboreshwa kasi ya ukuaji wa Uchumi itashuka zaidi na inaweza hata kufikia ukuaji hasi ( negative growth)”. Kimombo IMF waliandika “ If the policies weighing on the economy are not revised urgently, the pace of the country's economic growth may decline further or even lead to negative growth and potential risks to the balance of payments and debt sustainability". ‬


‪Hali ya ukuaji wa Uchumi wetu itaendelea kuwa mbaya kabla ya kuboreka Kwa sababu nishati ya kukuza uchumi inakauka; ‬

- ‪Mauzo Nje yameshuka sana. Mfano dhahiri ni Korosho mwaka 2018 ( Tanzania imepoteza USD milioni 500 ), Mbaazi mwaka 2017 ( Tanzania imepoteza USD milioni 250 ), Bidhaa za Viwanda 2017 na 2018 ( Rais Magufuli alipokea kijiti Cha Urais Tanzania ikiwa inauza Bidhaa za Viwanda Nje za thamani ya USD Bilioni 1.3, sasa hivi tunauza USD milioni 700 tu ).   Urari wa Malipo ya Bidhaa na Huduma umeongezeka mpaka nakisi ya USD milioni 680 mpaka Machi 2019. Mwaka unaoishia Machi 2016, Urari wa malipo ( overall balance of payments) ulikuwa na nakisi ya USD milioni 241 tu. ‬
- ‪Wafadhili wamezuia misaada na hivyo kuathiri utekelezaji wa Bajeti. Nchi mbalimbali zilizokuwa rafiki wa Tanzania zimezuia fedha za kigeni walizopanga kuipa Tanzania ili kutekeleza miradi mbalimbali. Hata taasisi kama Benki ya Dunia wamezuia Fedha kuja Tanzania. Fedha ambazo zimezuiliwa ni pamoja na ambazo zinapaswa kufadhili miradi ya kuboresha Elimu ya Sekondari SEQIP ( USD 400m Sawa shilingi Bilioni 920 ) TASAF III ( USD 300m Sawa na shilingi Bilioni 660 ) na Mradi wa Maji Vijijini ( USD 300m Sawa na shilingi Bilioni 660 ). Fedha hizi zimezuiwa Kwa sababu ya Serikali kutunga sheria kandamizi ya Takwimu kwa lengo la kumdhibiti Zitto Kabwe Lakini madhara yake kwa nchi ni makubwa mno. Kukosa MAARIFA kunaiathiri nchi. Sababu nyingine ‬Ni ubinywaji wa Demokrasia nchini, msingi wake Mkuu ukiwa ni kuporwa kwa ushindi wa Maalim Seif Sharif Hamad Katika Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa mwaka 2015. Kisha vitendo vya kuzuia Bunge Live, kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa vya Upinzani (ya CCM ikiruhusiwa), na kuwabambikia kesi mbalimbali wanasiasa wa upinzani, kupigwa risasi kwa Mbunge Tundu Lissu akiwa kwenye eneo la Bunge, na Kutungwa kwa sheria mpya ya vyama vya siasa inayoua kabisa siasa za vyama vingi nchi. Mfululizo wa matukio hayo yanayoua Demokrasia yetu umepelekea Nchi Wahisani (wafadhili) kutoleta fedha za kigeni nchini. Pia uminywaji huu wa Demokrasia pamoja na matukio mengine ya ukandamizwaji wa haki za binadam vimesababisha mahusiano ya Tanzania na nchi zinazofadhili na kuchangia Bajeti na hata mashirika ya kimataifa kudorora. Baadhi ya mashirika na nchi zikifuta kabisa misaada na huku wengine wakizuia au kuchelewesha kutoa fedha za kusaidia bajeti yetu ya Maendeleo. 
- Kupungua kwa Uwekezaji nchini ( FDI ) kunapekelea shughuli za Uchumi kutoongezeka, kutozalisha ajira rasmi za kutosha na kutoongeza Mapato ya Serikali. Taarifa ya Benki ya Dunia ( Economic Update No. 11 ) inaonyesha Kuwa Uwekezaji kwa uwiano wa Pato la Taifa ( GDP ) umeshuka kutoka 5% ya GDP mwaka 2015 mpaka 2% ya GDP mwaka 2018. Hii maana yake ni kuwa jumla ya shilingi Trilioni 4 zimeondoka kutoka Uchumi wetu Katika kipindi Cha miaka 3 tu. 

‪Hizo 3 ( Mauzo Nje, Wafadhili na Uwekezaji Mitaji ( FDI ) ) Ndio nishati ya kuendesha ukuaji wa Uchumi. Ni kama Gari na Mafuta ya Dizeli, unaweza kuwa na gari jipya Lakini halina mafuta, halitafika popote. Pia gari hiyo ikiwa na mafuta kidogo haitakufisha mbali unakokwenda. Kasi ya ukuaji wa Uchumi wetu imeporomoka Kwa sababu Serikali ya CCM ya Awamu ya 5 chini Rais John Magufuli inakata nishati ya kuendesha Uchumi kwa kuweka Sera fyongo. Mafuta yanayotumika kuendesha Uchumi wetu Hivi sasa yamechakachuliwa ( adulterated fuel ) ‬

‪Serikali inadhani kuwa mikopo ya kutoka mabenki ya Biashara ya Nje itaweza kuziba pengo la nishati niliyoeleza hapo juu, HAIWEZEKANI. Kwa Mfano Hivi sasa Serikali imekubaliana na Benki ya Standard Chartered kupata mkopo wa USD 1.5 Bilioni kwa ajili ya mradi wa Reli ( SGR ) na Benki ya Credit Suisse kupata mkopo wa USD 500 milioni kwa ajili ya miradi mingine ikiwemo Stiglers Gorge. Mikopo Hii ni ghali sana kwa riba na ni ya muda mfupi ( miradi inayofadhili itakuwa haijakwisha wakati mkopo unaanza kulipwa). Mikopo ghali kamwe haiwezi kuwa mbadala wa Nishati hizo 3. ‬

‪Rais Magufuli akubali tu kuwa amesimamia uharibifu mkubwa wa Uchumi wa nchi yetu na hivyo apishe watu wengine watakaoweza kurudisha Uchumi wetu kwenye Reli sahihi. Ni aibu kubwa kukabidhiwa nchi yenye Uchumi unaokua kwa 7 kwa miaka 10 mfululizo halafu wewe ndani ya miaka 3 unaupeleka Uchumi kwenye msinyao ( negative growth). Rais Magufuli na Baraza lake la Mawaziri hawapaswi kuwa Ikulu bali wanapaswa kuwa kizimbani kujibu mashtaka ya Uhujumu Uchumi ( economic sabotage ).

No comments :

Post a Comment