Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, July 17, 2019

BALOZI MPYA WA TANZANIA NCHINI CANADA AWASILI KUANZA KAZI!

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Mpoki Ulisubisya kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam tarehe Jumatatu Mei 20, 2019.

Balozi mpya wa Tanzania katika nchi ya Canada Mhe Dkt. Mpoki M. Ulisubisywa tayari ameshawasili nchini Canada.

Katika taarifa muhimu iliyotolewa na ubalozi wa Tanzania nchini Canada tarehe 17 mwezi wa July, ubalozi uliwafahamisha Wana-Diaspora wote kutoka Tanzania wanaoishi Canada kuwa balozi huyo aliwasili Ottawa, Canada tarehe 26 Juni, 2019. 

"Kwa sasa Mhe. Balozi anakamilisha baadhi ya taratibu zinazotakiwa, na baada ya taratibu hizo kukamilika, Ubalozi utawajulisha siku ambayo Mhe. Balozi atakutana nanyi kwa lengo la kufahamiana", ilielezea taarifa hio.

Taarifa hio muhimu iliendelea kueleza kuwa..."Kwa utangulizi tu, Mhe. Balozi anatanguliza shukrani zake za dhati kwa Wana-Diaspora wote kwa ushirikiano uliopo kati yenu na Ubalozi. Aidha, anathamini na kutambua mchango wenu mkubwa wa hali na mali mnaoutoa kwa ajili ya nchi yetu na Watanzania walioko nyumbani. Hivyo basi, ni matumaini ya Mhe. Balozi kuwa, ushirikiano huo 
tutauendeleza ili kwa pamoja tuijenge nchi yetu na tusaidie ndugu zetu".

Mwisho ubalozi uliwatakia majukumu mema na msimu mwema wa Kiangazi Wana-Diaspora wote nchini Canada.

Kama inavyojulikana kuwa Balozi Mpoki amechukuwa nafasi ya Bw. Alphayo Kidata ambae alitumbuliwa tarehe 8 November, 2018, ikiwa ni muda mfupi tu baada ya kufika Canada kuchukuwa nafasi yake ya kazi.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshuhudia Dkt. Mpoki Ulisubisya akiweka sahihi baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 20, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhi nyenzo za kazi Dkt. Mpoki Ulisubisya baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 20, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshuhudia Dkt. Mpoki Ulisubisya akila kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam  Jumatatu Mei 20, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza Mzee Ulisubisya Mwasumbi baba mzazi wa Dkt. Mpoki Ulisubisya baada ya kumuapisha mwanae kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam  Jumatatu Mei 20, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mke wa Dkt. Mpoki Ulisubisya baada ya kumuapisha mumewe kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 20, 2019. Wengine ni Baba na wana familia ya Balozi huyo mpya. (Picha na Ikulu).

No comments :

Post a Comment