Rais wa Iran Hassan Rouhani amedokeza kuwa huenda Iran ikaiachia meli iliyo na bendera ya Uingereza iwapo Uingereza itachukua hatua kama hiyo kwa kuiachia meli ya mafuta ya Iran iliyokamatwa Gibraltar mapema mwezi huu.
Rouhani ameyasema haya leo katika mkutano wa kawaida wa baraza la mawaziri."Hatutafuti kuendeleza mizozo na baadhi ya nchi za Ulaya.
Iwapo watadhamiria kuheshimu mifumo ya kimataifa na waache mambo mabaya wanayoyafanya ikiwemo kile walichokifanya Gibraltar, watapata jawabu sawia kutoka kwa Iran kutokana na kitendo chao.

"Kwa mara nyengine Iran imekataa kwamba yoyote kati ya ndege zake zisizo na rubani zilizuiwa baada ya Marekani kusema kuwa ilizilenga ndege zake mbili za aina hiyo wiki iliyopita. Waziri wa ulinzi wa Iran, Jenerali Amir Hatami amesema Marekani inastahili kutoa uthibitisho wa shambulizi kwa kuwa Iran ilitoa picha ilipoilenga ndege isiyo na rubani ya Marekani mwezi uliopita.

No comments :
Post a Comment