Hatua ya Iran kuikamata na kuendelea kuishikilia meli ya mafuta ya Uingereza inaleta changamoto na mtihani wa utiifu kwa waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson.
Waziri mkuu mpya wa Uingereza analazimika kuchagua kati ya kukubali meli katika eneo la ghuba kusindikizwa na vikosi vya Ulaya ama Marekani.
Ni upande gani Johnson anaweza kuelemea, utajenga hoja katika mada tete zinazomkabili ikiwa ni pamoja na kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya na kupata makubaliano ya kibiashara na Marekani.
Hatua atakazochukua zinaweza kuendeleza ama kuvunja juhudi za mataifa ya Ulaya kuweka hai makubaliano ya kudhibiti dhamira za Iran kujipatia silaha za kinyuklia ambapo Marekani imejitoa mwaka jana.
Baadhi ya wachambuzi nchini Marekani wanaiona hali hii kuwa ni changamoto kubwa kwa sera za Ulaya kuelekea Iran kwa jumla.

No comments :
Post a Comment