Mazungumzo ya kuitaka Korea Kaskazini kuachana na silaha za kinyuklia yako katika hatari kwa sababu Marekani inaonekana imo njiani kuvunja ahadi ya kutofanya luteka ya kijeshi na Korea Kusini.
Rais Donald Trump wa Marekani alionekana kufufua juhudi za kuishawishi Korea kaskazini kuachana na silaha za kinyuklia mwezi uliopita wakati alipokutana kwa muda mfupi na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un katika mpaka kati ya Korea mbili.
Trump alisema wamekubaliana kuanzisha tena kile kinachoitwa mazungumzo ya ngazi ya juu yaliyokwama tangu kuvunjika kwa mkutano wao wa tatu mwezi Februari.
Lakini msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Korea Kaskazini ameonesha shaka kuhusu hilo, akisema Marekani na Korea Kusini wanajitayarisha na mazoezi ya kijeshi yanayofahamika kama Dong Maeng katikati ya mwaka huu, ambayo ameyaita mazowezi kwa ajili ya vita.
No comments :
Post a Comment