Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, July 27, 2019

MUSIBA SASA AHAMIA KWA MARAIS WASTAAFU!


CYPRIAN Musiba, mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye amejipambanua kuwa mtetezi mkuu wa Rais John Magufuli, amewatuhumu watangulizi wa rais wa sasa, kuwa “waligeuza Ikulu kama danguro la kutafutia utajiri.” Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Alhamisi wiki hii, Musiba alisema, “ukimuondoa Mwalimu Julius Nyerere (rais wa kwanza wa Tanzania), wengine wote walioshika nafasi hiyo, “ni wezi watupu.”

“Marais wote wastaafu na wake zao, ukimuondoa Mwalimu Nyerere, walitumia Ikulu kujitajirisha,” amesema Musiba na kuongeza, “siwashambulii kwa sababu ninawachukia, kama ambavyo baadhi ya watu wanasema, ninachoeleza ndiyo ukweli halisi.”

Kuibuka kwa Musiba na kutuhumu viongozi wakuu wastaafu na wenza wao, kumekuja wiki moja tokea makatibu wakuu wawili wa zamani wa CCM, Kanali Abdulrahman Kinana na Luteni Yusuf Makamba, kulalamika kuchafuliwa.

Katika andishi lao la kurasa tatu kwa umma, Kinana na Makmba wamesema, kuna tishio la kumegeuka kwa chama hicho, kutokana na Musiba kushambulia viongozi wakuu wastaafu, baadhi ya mawaziri na watu wengine wenye mamlaka serikalini.


Kinana na Makamba wanadai kuwa “Musiba, pasipo kuwasilishwa ushahidi wowote amekuwa akituhumu kila mmoja kuwa wanataka kumhujumu Rais Magufuli, jambo ambalo linaoyesha kuna mfarakano unaoendelea ndani ya chama.”

Aidha, Kinana na Makamba wameelezwa kulifikisha sakata hilo mbele ya Katibu wa Baraza la Ushauri la Viongozi wakuu wastaafu, Pius Msekwa na mwenyekiti wake, Rais Ali Hassan Mwinyi.

Kutajwa kwa marais wastaafu na wenza wao, kumetafsiriwa na wachambuzi wa kisiasa kuwa, kumenogesha mjadala kuwa chini ya Musiba, hakuna aliyepo salama.

Katika kipindi cha uongozi cha Benjamin Mkapa, Mama Anna Mkapa alikuwa anaendesha Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF). Mpaka anaondoka madarakani, Desemba 2005, hajaelezwa fedha za kuendesha mfuko huo. Mama Mkapa ndiye mwenyekiti wa taasisi hiyo.

Mfuko wa Mama Mkapa, ulianzishwa mara baaada ya Rais Mkapa kuingia madarakani, Novemba 1995. Kwa muda wote ambao Mkapa alikuwa ikulu, mfuko huu ulikuwa unaendeshea shughuli zake katika majengo ya Ikulu.

Taarifa zinasema, hata gharama za bili ya maji, umeme, simu na mishahara ya wafanyakazi vililipwa na serikali. Misaada na michango iliyotolewa na wafadhili, mingi ilitolewa kwa kuwa mwenyekiti wake ni mke wa rais; mfuko ulionekana kama vile ni wa umma.

Akiongea kwa njia ya kumuingiza Mkapa katika dhahama, Musiba alisema, “tumuache Rais Magufuli afanye kazi. Hawa wengine wote walikuwa majizi. Watanzania wamepata rais ambaye hajawahi kutokea baada ya Mwalimu Nyerere.”

Anna Mkapa, anatajwa kuwa amejilimbikizia mali nyingi zenye thamani kubwa. Anatajwa kuwa yeye na mumewe, ndio wamilik wa mali nyingi za thamani.

Nao wake wa rais Mwinyi, Mama Sitti na Bi Hadija, walituhumiwa kugeuza Ikulu, kuwa pango la walanguzi. Katika kipindi cha utawala wake, ndipo wafanyabiashara kadhaa “waliingia Ikulu, bila kubisha hodi.”

Naye Salma Kikwete, mke wa rais Jakaya Kikwete, kama ilivyokuwa kwa Mama Anna Mkapa, alianzisha taasisi binafsi iitwayo, “Wanawake na Maendeleo (WAMA).

Mpaka sasa, hajaeleza  mabilioni ya shilingi aliyokusanya kupitia taasisi hiyo yametumika kwa kazi gani, huku kinachoitwa “maendeleo kwa wanawake wa Tanzania,” kikiwa hakionekani.

Musiba amekuwa akiwatuhumu viongozi hao na wengine wengine wandamizi, wakiwamo viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), kupanga njama za kumhujumu Rais Magufuli.

Makamba amekuwa katibu mkuu wa chama hicho kati ya mwaka 2007 hadi 2011. Alichukua nafasi hiyo, kutokea kwa Philip Mangula.

Naye Kanal Kinana alipokea wadhifa huo wa ukatibu mkuu kutokea mwaka 2012 hadi 2018, kutokea kwa Wilson Mukama; ambaye aliyehudumu nafasi hiyo kati ya mwaka 2011-2012. Kinana amepata kuhudumu pia kama Spika wa Bunge la Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa barua ya viongozi hao, inathibitisha hali si shwari ndani ya CCM.

“Tumetafakari kwa kina kabla ya kuamua kutoa taarifa hii kwa umma kuhusiana na uzushi alioutoa Cyprian Musiba dhidi yetu katika nyakati mbili tofauti,” inasema sehemu ya barua hiyo.

Tafsiri inayopatikana hapa ni kwamba kisiasa viongozi hawa wawili hawakutaka suala hilo liishie kwenye vikao vya ndani ya chama.

Kinana na Makamba wameonyesha kufahamu kinachoendelea na nani anamtuma mwanaharakati huyo kuwatuhumu. Hilo linathibitishwa na aya ya pili ya barua yao inayoeleza, “huyu anayetuhumu anatekeleza maagizo kama kipaza sauti.”

Barua inasema, “yeye anatumwa kutekeleza maagizo na kutumika kama kipaza sauti tu.” Sentensi hii peke inadhihirisha kuwa viongozi hawa wastaafu wana mengi mioyoni mwao ama wamechoshwa kukaa nayo pamoja na kuendelea kuvumilia kuchafuliwa na kuvunjiwa heshima kama walivyosema.

“Kwamba yupo mtu au kundi la watu ambao linamtumia mwanaharakati huyo kuwatuhumu viongozi wastaafu. Mantiki inatuelekeza kuwa Kinana na Makamba wanazo taarifa juu ya ‘mtu’ aliyeko nyuma ya harakati za zinazorushwa kwao, hivyo badala ya kuzitamka mwenyewe ameamua kutumia wakala.”

Barua ya Kinana na Makamba na kauli za Musiba, zimeibua makundi mawili – linalotetea makatibu hao wa Kikwete dhidi ya kundi jipya la kiongozi wa sasa wa nchi na CCM.

Makundi hayo mawili yamekuwa na kazi ya kulinda urithi mzuri wa viongozi wastaafu, huku lingine likiwa na wajibu wa kulinda maslahi ya mwenyekiti wa sasa wa CCM.


No comments :

Post a Comment