Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugora watatu kutoka kulia, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, Wabunge pamoja na Viongozi mbalimbali akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Nyumba za Makazi ya Askari Polisi katika eneo la Magogo mkoani wa Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro wakati akitoka kukagua moja ya nyumba za makazi ya Askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Magogo mkoani Geita.
Makamishna kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini wakifurahia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa sherehe za uzinduzi wa Nyumba za makazi ya Askari Polisi katika eneo la Magogo mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa nyumba za makazi ya Askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Magogo mkoani Geita.
Bendi ya Jeshi la Polisi ikitumbuiza katika sherehe za uzinduzi wa nyumba za makazi ya Askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Magogo mkoani Geita.
Sehemu ya Mradi wa nyumba za makazi ya Askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Magogo mkoani Geita ambao umezinduliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika eneo la Magogo mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa Geita mara baada ya kuhutubia katika uzinduzi wa nyumba hizo za makazi ya Askari Polisi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Geita wakati akielekea kuzindua nyumba za Askari wa Jeshi la Polisi mkoani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Katoro na Buseresere hawaonekani pichani wakati akielekea Geita mjini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Bwanga wakati akitokea Chato mkoani Geita.
PICHA NA IKULU
No comments :
Post a Comment