Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, July 23, 2019

Rais Trump akanusha taarifa za Iran!

Rais Donald Trump wa Marekani amesema kuwa taarifa za Iran kudai kuwa imewakamata majasusi 17 wanaofanya kazi katika Shirika la Ujasusi la Marekani, CIA, ni za uongo.

Trump ameyaandika hayo leo katika ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, akisema taarifa hizo za Iran hazina ukweli wowote.

Mapema leo mkuu wa idara ya kupambana na ujasusi ya Iran, alisema kuwa nchi yake imeugundua mtandao wa majasusi wa Marekani walioko Iran na imewakamata majasusi 17 wote wakiwa raia wa Iran.
Baadhi ya waliokamatwa huenda wakahukumiwa adhabu ya kifo. Trump amebainisha kuwa taarifa hizo ni za uongo na propaganda kama ilivyodai kuwa imeidungua ndege isiyokuwa na rubani.

No comments :

Post a Comment