Juzi waziri wa mambo ya nje wa Kenya bi Amina Mohamed alifika Tanzania kuturejeshea dhahabu yetu iliyokamatwa Kenya pamoja na pesa zilizoibiwa Tanzania tokea 2004.
Wengi wetu tulifurahia gesture hio ya majirani zetu Wakenya, lakini hatukufahamu the deeper meaning of their action, which is not that elusive.
Wakenya hawakuturejeshea dhahabu na pesa taslim, bali wametupiga kofi usoni (slapped us in the face) na zaidi wametuonesha uungwana na ustaarabu na vipi majirani wema wanatakiwa kuishi.
Tumesahau Watanzania tulivyowauza ng'ombe wao kutokana na sheria ya nchi yetu?
Suala la kujiuliza sasa hivi ni kuwa, je, kama dhahabu na pesa taslim za Kenya zingelikamatwa Tanzania, sisi Watanzania tungelimtuma waziri wetu wa mambo ya nje Bw. Kabudi awarejeshee Wakenya dhahabu yao na pesa zao au tungelisema kuwa kiendacho kwa mganga hakirudi na tungelitaifisha kila kitu?
Ikiwa ng'ombe hatukuwarejeshea, who in his proper senses would be inclined to believe kwamba dhahabu na pesa tungeliwarejeshea, especially during these economically hard times.
Wakenya wametusomesha Watanzania somo moja kubwa sana la kimaisha na ni lazima tusome na tubadilishe sheria zetu ili tukae na majirani zetu kwa wema na amani, kama wao walivyotufundisha hivi juzi.
Ingelikuwa kila kiingiacho nyumbani kwako ni halali yako, basi sisi wajane tungelikuwa tunafaidi!
Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment