Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, July 25, 2019

Ujerumani, Ufaransa, Uingereza na Uhispania zaijia juu Israel!

Ujerumani, Ufaransa, Uingereza na Uhispania zimekemea hatua ya Israel kubomoa nyumba za Wapalestina Mashariki mwa Yerusalem.

Nchi hizo nne zimetoa taarifa ya pamoja kwamba zinaishutumu Israel kwa kufanya uharibifu kwa nyumba za Wapalestina Yerusalemu Mashariki.

Katika taarifa iliyoandikwa kutoka Wizara ya Mambo ya nje ya Uhispania, Ujerumani, Ufarans na Uingereza, nchi zo zimekemea kubomolewa  kwa nyumba za Wapalestia katika Bonde al-Humus.
"Ubomoaji wa majengo katika maeneo yaliyokaliwa ni kinyume cha Sheria ya Kimataifa ya Binadamu na Maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na ni jambo la kuumiza kwa watu wa Palestina " ilisema taarifa hiyo.

Urusi, wakati huo huo, imeitaka Israeli iachane na uharibifu wa nyumba za Wapalestina Yerusalemu Mashariki.

No comments :

Post a Comment