Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, July 25, 2019

Waitara awatolea uvivu wanaoihujumu CCM!

Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Mwita waitara amewaonya wanaccm wanaoendelea kukihujumu chama cha mapinduzi angali bado ni wanachama huku wakijua hawakitendei haki chama hicho.

Waitara akiwa mkoani Njombe amesikitishwa na kitendo cha baadhi ya wanachama wa aina hiyo kwa kuwa wamekuwa wakijaribu kurudisha nyuma jitihada za kuyafikia maendeleo ya chama hicho.

“Hauwezi kuwa mbunge wa chama cha mapinduzi,unaingia kwenye vikao vya ccm vya chama halafu unapinga serikali huko nje na chama chake hauwezi kuwa,ukitaka ubaki salama kama wewe na maisha yako utakufa,wenzetu ulaya huwa wanaua nenda china kafanye mambo hayo”amesema Waitara.Waitara ameongeza kuwa

“kwa hiyo huwezi kuwa mbunge wa chama cha mapinduzi,unakaa kwenye vikao vya chama,watu wanapanga mikakati halafu ukiwa mtaani unatoa yote,unatuhujumu ni kama tupo kwenye mtumbwi tunaogelea unatoboa inatakiwa tukuwahi ili uzame wewe tusizame wote ili tubaki salama”alisema Waitara

Akizungumzia upande wa watumishi wa umma waziri huyo ametoa wito kumuunga mkono rais Magufuli kutokana na juhudi kubwa anazozifanya kwa watanzania.

“kwa mtu mstaarabu anayejua uongozi maana yake nini,siwezi kukubali uteuzi nikaenda nikala kiapo,nikapewa majukumu,nikapewa na gari nikapewa na posho nikapewa na mshahara halafu nikaka kwenye vijiwe nikamtukana rais hivi unakuwa unaakili kweli,sasa watu ambao wanashangaa hivi watu wanaondolewa uongozi wewe hujui utaratibu”alisema tena Waitara

No comments :

Post a Comment