Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, July 24, 2019

Waziri wa mambo ya nje wa Iran ampongeza Waziri Mkuu mpya wa Uingereza!

Waziri wa mambo ya nje wa Iran amempongeza Boris Johnson kwa kushinda kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya kuwa waziri mkuu mpya wa Uingereza na kuionya Uingereza kwamba nchi yake italilinda eneo la ghuba.

Mohammed Javad Zarif ameandika ujumbe wa Twitta na kumpongeza waziri mwenzake wa zamani wa mambo ya nje Boris Johnson kwa kuchaguliwa mnamo wakati ambapo kuna mvutano kati ya nchi hizo mbili kuhusu kukamatwa kwa meli za mafuta.

Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu amesema Iran haitafuti makabiliano lakini inalilinda eneo la ukubwa wa maili 1500 la pwani ya Ghuba ya uajemi.
Ijumaa iliyopita walinzi wa mapinduzi ya Iran waliikamata meli iliyokuwa na bendera ya Uingereza ambayo ni mshirika wa Marekani.

No comments :

Post a Comment