Mhe. Balozi Wilson. M. Masilingi alitembelewa na vijana kutoka Tanzania na kuongea nao katika ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Washington, D.C. Vijana hao wamemaliza ziara yao iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani iitwayo "Mandella Washington Fellowship for Young African Leaders". Mhe. Balozi Wilson Masilingi aliwapongeza na kuwashauri kutumia fursa waliyopewa kushiriki Programu hii kuleta maendeleo nchi yetu kwa kushiriki ujenzi wa uchumi wa viwanda na kuongeza ajira kwa vijana. Aidha aliwaasa kuwa Wazalendo na kulinda uhuru na Demokrasia katika nchi yetu.
Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment