dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, August 22, 2019

Rais wa Iran asema njia za kimataifa baharini hazitokuwa salama!

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema kuwa kama Iran haitoweza kuuza mafuta yake kabisa, njia za kimataifa za kupitia meli za kibiashara hazitakuwa na usalama kama ilivyokuwa siku za nyuma.

Rouhani ameyasema hayo wakati akiionya Marekani dhidi ya kuiongezea Iran mbinyo katika makabiliano makali kati ya maadui hao wa muda mrefu. Kauli hiyo ya Rouhani imeenda sanjari na matamshi ya Waziri wa Mambo ya kigeni wa Iran Mohammad Javad Zarif kuwa Iran huenda ikachukua hatua zisizotabirika katika kujibu sera zisizotabirika za Marekani chini ya Rais Donald Trump.


Rais huyo wa Iran aliyasema hayo wakati akikutana na Kiongozi wa Juu Ayatollah Ali Khamenei. Mvutano kati ya Marekani na Iran umeongezeka tangu utawala wa Trump ulipojiondoa katika mkataba wa kimataifa wa kudhibiti mipango ya nyuklia ya Iran na kuanza kuiongezea vikwazo.

No comments :

Post a Comment