Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, October 6, 2019

Askari Sita Wakuhumiwa Kwa Kuiba Mafuta ya Ndege!

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu askari sita akiwemo wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) kulipa faini ya Sh 500,000 kila mmoja bada ya kukiri shtaka la wizi wa mafuta ya ndege (Jet A-1/Ik).

Askari hao ni Koplo Shwahiba(38), MT. 74164 SGT Ally Chibwana (47) wa JWTZ, PC Elidaima Paranjo (38), PC Simon (28), PC Dickson na PC Hamza Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi, Vick Mwaikambo baada ya washtakiwa hao kukiri shtaka linalowakabili.

Mwaikambo alisema kwa kuwa washtakiwa hao ni kosa lao la kwanza hivyo mahakama hiyo imewapa adhabu ya kulipa faini hiyo kila mmoja na madumu 109 yenye mafuta hayo yatarudishwa serikalini.

Awali wakili wa Serikali Mwandamizi, alidai kuwa awali washtakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na makosa matatu hivyo walikubaliana kuliondoa shtaka la kwanza la kupanga genge la uhalifu na shtaka la tatu ni la utakatishaji wa fedha na shtaka la pili la wizi limebaki.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa Julai 30, mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam, waliiba lita 2180 za mafuta ya ndege (Jet A-1/Ik) yenye thamani ya Sh 4,647,760 mali ya ATCL.
 GPL

No comments :

Post a Comment