Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, October 3, 2019

Baba yake Beyonce afichua kuwa aligundulika na saratani ya matiti!


Mathew Knowles, baba yao wanamuziki maarufu wa wanamuziki wa pop Beyonce na Solange Knowles, amefichua kuwa alipatikana na ugonjwa wa saratani ya matiti.

Bwana Knowles mwenye umri wa miaka 67-amezungumzia kuhusu hali yake katika mahojiano na kipindi cha Good Morning America, ambacho kitatangaza mahojiano hayo baadae leo katika kituo cha wa televisheni nchini Marekani cha ABC.

Kionjo cha mahojiano kilitumwa Jumanne kuambatana na siku ya kwanza ya mwezi wa kutoa uelewa juu ya saratani.


Saratani ya matiti ambayo ni nadra kwa kawaida hutokea kwa wanaume wenye umri wa zaidi ya miaka 60.

Katika kionjo hicho cha mahojiano, Bwana Knowles ameonyeshwa akiulizwa ni jinsi gani alitangaza kwa mara ya kwanza taarifa ya ugonjwa huo kwa familia yake.

Bwana Knowles ambaye ni mjasiliamali na msemaji wa umma amesema kuwa "atatoa tangazo maalum " katika kipindi cha Jumatano.

Knowles, ambaye ni afisa mauzo wa zamani katika kampuni ya Xerox anafahamika zaidi kwa kuunda kikundi cha bendi ya Destiny's Child, bendi ambayo illimuinua binti yake mkubwa Beyonce hadi kufikia kiwango cha kuwa nyota kimuziki .Pia alikuwa meneja wa muziki wake wa solo hadi mwaka 2011

Alitalikiana na mama yake Beyonce na Solange Tina mwaka 2011 na tangu wakati huo alipata watoto wawili na mke wake wa pili Gena.

No comments :

Post a Comment