Wanadiplomasia wa Israel hii leo wameanza mgomo wa wazi usiokuwa na ukomo na kufunga balozi zaidi ya 100 pamoja na balozi ndogo kote ulimwenguni wakigomea mazingira ya kazi.
Mgomo huo unatokana na mzozo wa muda mrefu kati ya watumishi wa balozi na wizara ya fedha ambayo kulingana na watumishi hao imekuwa ikibadilisha sheria zinazohusu urejeshwaji wa fedha zinazotumika kuwahudumia na kuwaburudisha wageni wa kikazi.
Chama cha watumishi wa wizara ya mambo ya nje kimesema kwenye taarifa yake kwamba wanalazimika kufunga balozi kote duniani kuanzia hii leo na hakuna huduma itakayotolewa kwa umma na wageni hawataruhusiwa kuingia kwenye balozi hizo.
No comments :
Post a Comment