dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, October 3, 2019

Mchezaji aliyenusurika ajali ya Ndege iliyoua watu 71 afunga goli lake la kwanza!


Ajali ya ndege ya LaMia 2933 iliyokuwa imebeba wachezaji wa klabu ya soka ya nchini Brazil ya
 Chapecoense iliyotokea Novemba 28 2016 ni moja kati ya matukio kubwa la kihistoria katika soka toka karne ya 21 ianze.

Ndege hiyo ilikuwa imebeba watu 77 wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na wahudumu wa ndege wakitoka Brazil kwenda Colombia katika mchezo wa fainali wa Klabu Bingwa Amerika Kusini (Sudamericana) na walinusurika sita kati ya 77 akiwemo mchezaji Alan Ruschel.


Ruschel ,30, ndio miongoni mwa manusura waliopona na kufanikiwa kurejea uwanjani kucheza soka tena Agosti 7 2017 ,lakini ilimchukua muda mrefu kufunga goli hadi Septemba 30 2019 akifunga bao la ushindi 1-0 dhidi ya Cruzerio akiichezea Goias kwa mkopo akitokea Chapecoense aliyokuwa nayo wakati inapata ajali katika kijiji cha Cerro Gordo nchini Colombia.

No comments :

Post a Comment